Monday, December 12, 2016

BABU WA MIAKA 81 ATAFUTA KLABU YA KUKIPIGA UINGEREZA

Babu atafuta klabu mpya ya kuchezea Uingereza

Dickie BorthwickMchezaji kandanda wa umri wa miaka 81, anayeaminika kuwa mchezaji soka mkongwe zaidi nchini Uingereza, anatafuta klabu mpya.
Dickie Borthwick, anayetoka Weymouth, Dorset, alianza kucheza kandanda mwaka 1947 akiwa na miaka 12.
Alikuwa mchezaji katika klabu ya wanajeshi wastaafu ya Wyke kabla ya klabu hiyo kuvunjwa. Hata hivyo, anakiri kwamba huenda umri umemzidi na haitamfaa kucheza kwenye ligi ya wanajeshi wastaafu tena.
ALiambia gazeti la The Mirror nchini Uingereza kwamba amepokea mwaliko wa kujiunga na klabu ya soka ya matembezi lakini amesema anataka kushiriki soka yenye kasi kiasi.
BBC

No comments:

Post a Comment