Saturday, October 31, 2015

CHALSEA YABAGWA , MAN YAAMBULIA SARE


MATOKEO LIGI KUU YA ENGLAND JANA
Crystal Palace 0-0 Manchester United
Swansea City 0-3 Arsenal
West Bromwich 2-3 Leicester City
Newcastle United 0-0 Stoke City
Watford 2-0 West Ham United
Manchester City 2-1 Norwich City
Chelsea 1-3 Liverpool
Leo ; Novemba 1, 2015
Everton Vs Sunderland (Saa 10:30 jioni)
Southampton Vs Bournemouth (Saa 1:00 usiku)
J’tatu Novemba 2, 2015
Tottenham Hotspur Vs Aston Villa (Saa 5:00 usiku)


TIMU ya Arsenal imeendelea ‘kula sahani moja’ na Manchester City kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Swansea City jioni ya jana Uwanja wa Liberty.
Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Olivier Giroud dakika ya 49, Laurent Koscielny dakika ya 68 na Joel Campbell dakika ya 73 na sas Arsenal inafikisha pointi 25 sawa na Man City baada ya timu kucheza mechi 11, ingawa inabaki nafasi ya pili kwa kuzidiwa wastani wa mabao.
Michezo mingine ya ligi hiyo , Crystal Palace imelazimishwa sare ya 0-0 na Manchester United Uwanja wa Selhurst Park sawa na Newcastle United na Stoke City Uwanja wa St. James' Park.
Leicester City imeshinda ugenini 3-2 dhidi ya West Bromwich Albion Uwanja wa The Hawthorns mabao yake yakifungwa na Riyad Mahrez dakika ya 57 na 64 na Jamie Vardy dakika ya 77, wakati ya wenyeji yamefungwa na Salomon Rondon dakika ya 30 na Rickie Lambert kwa penalti dakika ya 84.

Mabao ya Odion Ighalo dakika ya 39 na 48 Uwanja wa Vicarage Road yameipa Watford ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham United, wakati Manchester City imeshinda 2-1 dhidi ya Norwich City Uwanja wa Etihad, mabao yake yakifungwa na Nicolas Otamendi dakika ya 67 na Yaya Toure kwa penalti dakika ya 89, huku la wageni likifungwa na Cameron Jerome dakika ya 83.
Mchezo uliotangulia jioni ya leo, Chelsea imeendelea kuboronga baada ya kufungwa 3-1 nyumbani Uwanja wa Stamford Bridge na Liverpool.

Ramires Santos do Nascimento alianza kuifungia The Blues dakika ya nne, kabla ya Philippe Coutinho kuisawazishia Liverpool dakika ya 48 na kuifungia la pili dakika ya 74, huku la tatu likifungwa na Christian Benteke dakika ya 83.
Winga wa zamani wa Man United, Zaha akijaribu kupasua katikati ya wachezaji wa timu hiyo, Marcos Rojo na Morgan Schneiderlin

MABOMU YARINDIMA MKWAKWANI


Penalti iliyofungwa na Raphael Alpha imezua tafrani kubwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga wakati wa mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara.

Kiungo huyo wa Mbeya City alifunga penati hiyo ya dakika ya 90 baada ya Coastal Union kuongoza kwa muda wote.
Hali hiyo ilifanya mashabiki wa Coastal Union kufanya vurugu kubwa ikiwa ni pamoja na kuharibu ubao wa kubadilishia wachezaji, pia ripoti za mwamuzi wa akiba.
 
Polisi walilazimika kuingiza gari katikati ya uwanja na kupambana na mashabiki hao kwa kupiga mabomu ya machozi.

Mashabiki hao waliendelea kurusha mawe wakiwapiga waamuzi ambao walipewa ngao ya Polisi kujilinda wakiwa katika gari la Polisi.







CHALSEA BADO YAENDELEZA UTEJA UINGEREZA

Full Time ya Chelsea Vs Liverpool

Ligi Kuu soka Uingereza imeendelea tena October 31, kwa michezo kadhaa kupigwa wakati klabu ya Chelsea ya Uingereza iliyochini ya kocha wa kireno Jose Mourinho iliwakaribisha majogoo wa jiji Liverpool katika dimba la Stamford Bridge kucheza mechi yake ya 11 katika Ligi.
P151031-027-Chelsea_Liverpool-1200x806
Chelsea iliingia uwanjani ikiwa na presha ya rekodi mbovu ambayo imetokana na kutokufanya vizuri katika mechi zake kumi za mwanzo kwani ilikuwa imeshinda mechi tatu, sare mechi mbili na kufungwa mechi tano, hiki ni kipindi kigumu kwa Chelsea ambayo ni Bingwa mtetezi wa Ligi hiyo licha ya kuwa yupo katika nafasi za chini katika msimamo wa Ligi.
Football - Chelsea v Liverpool - Barclays Premier League - Stamford Bridge - 31/10/15 Ramires celebrates after scoring the first goal for Chelsea Action Images via Reuters / John Sibley Livepic EDITORIAL USE ONLY. No use with unauthorized audio, video, data, fixture lists, club/league logos or "live" services. Online in-match use limited to 45 images, no video emulation. No use in betting, games or single club/league/player publications. Please contact your account representative for further details.
Hata hivyo mechi imemalizika kwa klabu ya Chelsea kukubali kupokea kipigo cha goli 3-1 na kuendelea kuweka mashakani kibarua cha kocha wao Jose Mourinho. Magoli ya Liverpool yalifungwa na Philippe Coutinho dakika ya 45 na 74 huku Christian Benteke akikamilisha goli la tatu dakika ya 83, Chelsea walipata goli la kufutia machozi dakika ya 4 ya mchezo kupitia kwa Ramires.

HADI MAPUMZIKO SIMBA 4 MAJIMAJI 0

TUNACHANJA MBUGA TU


Simba imeamka, hadi mapumziko inaongoza kwa mabao 4-0 dhidi ya Majimaji ya Songea.


Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kiungo Ibrahim Ajibu amefunga mabao matatu 'hat trick' huku mshambuliaji Hamisi Kiiza akifunga moja.

Majimaji wanaonekana kupoteana kabisa na kama watacheza hivyo kipindi cha pili wanaweza kulala hata mabao saba au zaidi.

WATU ZAIDI YA 200 WADAIWA KUPOTEZA MAISHA BAADA YA NDEGE KUANGUKA,EGYPT

Ndege imeanguka Egypt na watu zaidi ya 200… chanzo? vifo? hiki ndio kilichonifikia

Ajali za ndege huwa ni chache sana ukiinganisha na ajali za usafiri mwingine kama magari na meli, hiyo sina imefanya usafiri wa ndege kupewa namba moja ya usafiri salama zaidi Duniani kwa muda mrefu !!
Ndege ya abiria iliyokuwa inamilikiwa na Russia imeripotiwa kupata ajali saa chache zilizopita, kulikuwa na ripoti tofauti kuhusu usalama wa abiria 224 ambao walikuwa ndani ya Ndege hiyo lakini Ubalozi wa Russia uliopo Egypt wamethibitisha vifo vya wato wotw waliokuwa ndani ya ndege hiyo.
Plane Crush
Kati ya watu hao waliokuwemo, 217 ni raia wa Russia, pamoja na wafanyakazi saba ambao walikuwa wakihudumia ndani ya ndege.
Ndege hiyo ilitoka Egypt ikielekea St. Petersburg, Russia… ndege ilipotea kuonekana kwenye rada na muda mfupi baadae ikaanguka eneo la Sinai.

COASTAL UNION NA MBEYA CITY, MKWAKWANI, TANGA

 Hadi mapunziko Coastal Union inaongoza bao 1 lililofungwa na Nassour Kipanga ambapo kipindi hicho Mbeya ilikosa mabao 2 ya wazi. Hata hivyo Coastal Union inajibabadua na kuonekana kuzidiwa kwa kiwango kikubwa.
Safu ya uashabuliaji inadaiwa kuwa butu na hivyo kushindwa kuwapa raha washabiki.
Fuatilia blog hiii kuona dakika 90 itakuwaje ni hapahapa tangakumekuchablog









JOSE MOURINHO MGUU MMOJA DARANI NA MMOJA BERNABEU

Jose Mourinho kurejea Real Madrid? Rais wa zamani wa Real Madrid kaongea haya…

Kwa sasa kocha wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Jose Mourinho anahusishwa na kutaka kufutwa kazi endapo tu atapoteza mchezo dhidi ya Liverpool licha ya kuwa taarifa hizo sio rasmi. October 30 mtandao wa mirror.co.uk uliripoti kuwa klabu ya Real Madrid ya Hispania inamuhitaji Jose Mourinho arudi kuifundisha timu yao sambamba na kuombwa hamshawishi Eden Hazard kwenda Real Madrid.
October 31 Rais wa zamani wa Real Madrid ya Hispania Ramon Calderon amesema kuwa Jose Mourinho anakaribishwa tena Santiago Bernabeu kauli ambayo inaongeza nguvu tetesi za kuwa Jose Mourinho huenda akarudi Hispania kuifundisha timu hiyo.
jose-mourinho-chelsea-lam-437576 (1)
Ramon Calderon alifika mbali zaidi kwa kusema kuwa kocha wa sasa wa klabu hiyo Rafael Benitez alikuwa chaguo la nne baada ya Jose Mourinho, Joachim Low na Jurgen Klopp  kuhusishwa kutaka kuingia mkataba wa kutaka kuifundisha timu hiyo katika msimu wa 2015/2016.
Real Madrid's new President Ramon Calderon unveils Fabio Capello as the new manager of Spanish football club Real Madrid at the Santiago Bernabeu in Madrid, 06 July 2006. Capello signed a three year contract with Real and is expected to try and strengthen Madrid's midfield by targeting Lyon's Malian Mahamadou Diarra and Brazil's Emerson of Juventus in an attempt to end their three trophyless seasons. AFP PHOTO/PIERRE-PHILIPPE MARCOU
Ramon Calderon 
“Kiukweli Rafael Benitez alikuwa chaguo la nne kwa Real Madrid, nafikiri Perez bado anajaribu kutaka kumrudisha Mourinho Real Madrid, kiukweli anampenda, mimi sio shabiki wa Mourinho ila kwa rekodi aliyoiweka klabuni hapa kwa kipindi cha miaka mitatu sio vibaya akirudi” >>>Ramon Calderon
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

WANZANIBARI WAISHIO MAREKANI WATOA YA MOYONI

TAARIFA YA ZADIA KUHUSU KUFUTWA KWA MATOKEO YA UCHAGUZI ZANZIBAR.

Logo ya Zadia
Jumuiya ya Wazanzibari Waishio Nchini Marekani (ZADIA), imekuwa ikifuatilia kwa karibu na makini zaidi zoezi zima la Uchaguzi Mkuu visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Kwa kiasi kikubwa mchakato wa uchaguzi ulifanyika kwa njia za amani na utulivu. Hata hivyo ZADIA imeshtushwa mno na tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mh. Jecha Salim Jecha la kutangaza kuufuta Uchaguzi Mkuu Zanzibar na matokeo yake.
Ama kwa hakika kitendo hicho hakikuwa cha busara na kinapelekea kurudisha nyuma maendeleao ya demokrasia Zanzibar, na vilevile hakiashirii mustakbali mwema kwa nchi yetu tuipendayo. Wazanzibari wameelezea maoni na matakwa yao kwenye visanduku vya kupigia kura, na maoni na matakwa yao hayo yanapaswa kusikilizwa na kuheshimiwa.
Kwa hivyo, ZADIA inatoa wito kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar, kumalizia mchakato mzima wa kuhesabu kura kwa majimbo yaliyobakia na kutoa matokeo ya mwisho ya Uchaguzi na kumtangaza mshindi ili kuiepusha Zanzibar yetu tuipendayo kuingia katika hali ya mtafaruku na mifarakano isiyokuwa na tija bali kuleta hasara.
ZADIA pia inaungana na jumuiya zote za kimataifa ambazo zimetoa msimamo wao juu ya uchaguzi wa Zanzibar, hasa ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, ambao ni kiungo madhubuti kati ya Wazanzibari walioko Zanzibar na wenzao wanaoishi nchini Marekani.
Chanzo Full Shangwe

Friday, October 30, 2015

MAGAZETI TUNANGALIA

 Wakazi jijini Tanga wakiangalia magazeti kufuatilia habari za ushindi wa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli Leo.




JOSE MOURINHO AZIDI KUKALIA KUTI KAVU

Kwa mwenendo wa Chelsea vipi Jose Mourinho anafikiria watamaliza Top 4? hili ndio jibu lake…

Ikiwa masaa kadhaa yamesalia kabla ya klabu ya Chelsea ya Uingereza kucheza mechi na Liverpool katika uwanja wake wa nyumbani wa Stamford Bridge, huu utakuwa mchezo wa kumi na moja kwa Chelsea ambayo hadi sasa katika michezo kumi iliyocheza imefungwa mechi tano, imeshinda mechi tatu na kutoa sare mechi mbili na ipo nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza.
Kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho ambaye timu yake itacheza na Liverpool huku ikiwa na presha ya kutaka kuokoa kibarua cha kocha huyo ambaye anatajwa kama atapata matokeo mabovu katika mchezo huo, huenda akafukuzwa kazi, hata hivyo Mourinho ambaye ana maneno mengi ameshindwa kuthibitisha kuwa kama anaamini timu yake itamaliza katika nafasi nne za juu na kupata tiketi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu ujao.
2DF1F70E00000578-0-image-a-69_1446209906487
“Ni jinsi gani napambana na hii hali? ni kwa kufanya kazi sina mashaka tutatoka katika hiki kipindi kigumu mapema lakini siwezi kuahidi kuwa tutapata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao, na kuhusu ulazima wa kushinda hii mechi, kwa kazi yangu huwa sishindi kila mechi ila huwa ni lazima kushinda kwa kila mchezo”>>> Jose Mourinho
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

SOKA UWANJANI KESHO, UINGEREZA, SPAIN NA TANZANIA

Ratiba ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara, Uingereza na Hispania October 31 na November 1

Tukiwa bado katika muendelezo au mfululizo wa mechi mbalimbali za soka, naomba nikusogezee ratiba ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara, Uingereza na Hispania zitakazochezwa weekend hii, Ligi Kuu Tanzania bara October 31 na November 1 kutakuwa na jumla ya mechi nane, baada ya hapo Ligi Kuu Tanzania bara itasimama hadi December 12 hii inatokana na kupisha maandalizi ya mechi ya Algeria na michuano ya Kombe la Chalenji. Hii ni ratiba ya mechi za Ligi Kuu Tanzania, Uingereza na Hispania kwa mechi za October 31 na November 1.
vpl
Ratiba ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara weekend hii zitachezwa saa 16:00
epl
Ratiba ya Ligi Kuu Uingereza kwa saa za Afrika Mashariki October 31
  • Chelsea Vs Liverpool  Saa 15:45
  • Crystal Palace Vs Man Utd  Saa 18:00
  • Man City Vs Norwich Saa 18:00
  • Newcastle Vs Stoke Saa 18:00
  • Swansea Vs Arsenal Saa 18:00
  • Watford Vs West Ham Saa 18:00
  • West Brom Vs Leicester Saa 18:00
Jumapili ya November 1
  • Everton Vs Sunderland Saa 16:30
  • Southampton Vs Bournemouth Saa 19:00
Laliga
Ratiba ya Ligi Kuu Hispania kwa saa za Afrika Mashariki Jumamosi ya October 31
  • Real Madrid Vs Las Palmas Saa 18:00
  • Valencia Vs Levante Saa 20:15
  • Villarreal Vs Sevilla Saa 20:15
  • Getafe Vs Barcelona Saa 22:30
  • Real Sociedad Vs Celta de Vigo  Saa 00:05
Jumapili ya November 1
  • Eibar Vs Rayo Vallecano Saa 14:00
  • Espanyol Vs Granada CF Saa 18:00
  • Sporting de Gijón Vs Málaga Saa 20:15
  • Real Betis Vs Ath Bilbao Saa 22:30
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

CHINA NA UZAZI WA MPANGO

China itaruhusu watu kuwa na watoto wawili? Huu ndio mpango mpya..


Kitendo cha Sheria za China kupiga marufuku watu kuzaa mtoto zaidi ya mmoja, ilikuwa ni kitu ambacho Mataifa mengi Duniani yalikuwa yakikipiga vita, good news kutoka huko ninayo, mambo yamebadilika japo kwa wengine wanasema bado haitoshi !!
Kwa sasa China ina jumla ya watu Bilioni 1.3 kutokana na Sera ya kila wanandoa kutakiwa kuwa na mtoto mmoja tu, lakini Serikali ya China imeona umuhimu wa utaratibu huo kubadilishwa ambapo kwa sasa wako wanandoa wanaruhusiwa kuwa na watoto wawili tu.
china_2268471b
Japo hii inaweza kuwa na kitu kizuri kwa raia wa China lakini Taasisi ya haki za binadamu Amnesty International wamesema bado haitoshi, wanahitaji Sheria iachiwe zaidi watu wawe huru kujiamulia idadi ya watoto wanaohitaji kuwa nao.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

Thursday, October 29, 2015

UCHAGUZI TANZANIA

UN TANZANIA STATEMENT ON TANZANIA GENERAL ELECTIONS

IMG_5569UN Resident Coordinator, Alvaro Rodriguez.
Dar es Salaam, 29 October 2015: The United Nations is following very closely the Tanzanian general elections of 25 October and congratulates the president elect. We congratulate Tanzanians for exercising their democratic rights in a peaceful manner. We take note of the international observers statement (Commonwealth, AU, SADC and EU) of today that indicates they are pleased that the voting and counting took place in an environment of peace.
However, the observer missions as well as the US Embassy and UK High Commission have also shared their great concern with the statement issued by the Chairman of the Zanzibar Electoral Commission in which he nullified the Zanzibar elections.
We call on political leaders to promote an environment of peaceful dialogue to resolve their differences and to ensure a continued peaceful and democratic elections process. It is through this peaceful and democratic process that the social and economic development of the United Republic of Tanzania can be ensured.
SIGNED BY: ALVARO RODRIGUEZ
UN RESIDENT COORDINATOR

FURAHA YA USHINDI WA CCM URAIS



Wakazi wa Tanga na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakishangilia mitaani mara baada kutangazwa mshindi Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.



TASWIRA YA TANGAKUMEKUCHA LEO JIJI LA TANGA

 Serikali imekuwa ikifanya kila jitihada za kuhakikisha inawaletea maendeleo wananchi ikiwa na pamoja na kuboresha miundombinu yake ikiwa ni kurahisisha huduma za kimaendeleo.
Mbali ya jitihada zake hizo lakini pia imekuwa ikizidiwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za hujuma za makusudi kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakikwamisha kwa maslahi yao binafsi
Jicho la Tangakumekuchablog katika kuangaza kwake imekutana na chemba eneo la Centre Bakery njia ielekeayo Idara ya Maji katikati ya jiji la Tanga.
Inadaiwa kuwa chemba hilo limekuwa kero kwa zaidi ya wiki mbili na mamlaka inayohusika kutochukua hatua zozote na hivyo kuwa kero