Friday, October 30, 2015

CHINA NA UZAZI WA MPANGO

China itaruhusu watu kuwa na watoto wawili? Huu ndio mpango mpya..


Kitendo cha Sheria za China kupiga marufuku watu kuzaa mtoto zaidi ya mmoja, ilikuwa ni kitu ambacho Mataifa mengi Duniani yalikuwa yakikipiga vita, good news kutoka huko ninayo, mambo yamebadilika japo kwa wengine wanasema bado haitoshi !!
Kwa sasa China ina jumla ya watu Bilioni 1.3 kutokana na Sera ya kila wanandoa kutakiwa kuwa na mtoto mmoja tu, lakini Serikali ya China imeona umuhimu wa utaratibu huo kubadilishwa ambapo kwa sasa wako wanandoa wanaruhusiwa kuwa na watoto wawili tu.
china_2268471b
Japo hii inaweza kuwa na kitu kizuri kwa raia wa China lakini Taasisi ya haki za binadamu Amnesty International wamesema bado haitoshi, wanahitaji Sheria iachiwe zaidi watu wawe huru kujiamulia idadi ya watoto wanaohitaji kuwa nao.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment