Saturday, October 31, 2015

JOSE MOURINHO MGUU MMOJA DARANI NA MMOJA BERNABEU

Jose Mourinho kurejea Real Madrid? Rais wa zamani wa Real Madrid kaongea haya…

Kwa sasa kocha wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Jose Mourinho anahusishwa na kutaka kufutwa kazi endapo tu atapoteza mchezo dhidi ya Liverpool licha ya kuwa taarifa hizo sio rasmi. October 30 mtandao wa mirror.co.uk uliripoti kuwa klabu ya Real Madrid ya Hispania inamuhitaji Jose Mourinho arudi kuifundisha timu yao sambamba na kuombwa hamshawishi Eden Hazard kwenda Real Madrid.
October 31 Rais wa zamani wa Real Madrid ya Hispania Ramon Calderon amesema kuwa Jose Mourinho anakaribishwa tena Santiago Bernabeu kauli ambayo inaongeza nguvu tetesi za kuwa Jose Mourinho huenda akarudi Hispania kuifundisha timu hiyo.
jose-mourinho-chelsea-lam-437576 (1)
Ramon Calderon alifika mbali zaidi kwa kusema kuwa kocha wa sasa wa klabu hiyo Rafael Benitez alikuwa chaguo la nne baada ya Jose Mourinho, Joachim Low na Jurgen Klopp  kuhusishwa kutaka kuingia mkataba wa kutaka kuifundisha timu hiyo katika msimu wa 2015/2016.
Real Madrid's new President Ramon Calderon unveils Fabio Capello as the new manager of Spanish football club Real Madrid at the Santiago Bernabeu in Madrid, 06 July 2006. Capello signed a three year contract with Real and is expected to try and strengthen Madrid's midfield by targeting Lyon's Malian Mahamadou Diarra and Brazil's Emerson of Juventus in an attempt to end their three trophyless seasons. AFP PHOTO/PIERRE-PHILIPPE MARCOU
Ramon Calderon 
“Kiukweli Rafael Benitez alikuwa chaguo la nne kwa Real Madrid, nafikiri Perez bado anajaribu kutaka kumrudisha Mourinho Real Madrid, kiukweli anampenda, mimi sio shabiki wa Mourinho ila kwa rekodi aliyoiweka klabuni hapa kwa kipindi cha miaka mitatu sio vibaya akirudi” >>>Ramon Calderon
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment