Saturday, October 17, 2015

TUME YA UCHAGUZI TAIFA YASIKITISHWA NA MANENO MAKALI JUKWAANI




Tangakumekuchablog
Tanga, KAMISHNA wa Tumeya Taifa ya Uchaguzi, Mjaka Mchanga, amesikitishwa na mwenendo wa kampeni za uchaguzi majukwaani na kuwaomba wagombea kuacha kutoa maneno makali na badala yake kutangaza sera za vyama vyao.
Akizungumza katika kongamano leo na viongozi wa vyama vya siasa ukumbi wa mikutano jengo la Mkuu wa Mkoa, Mchanga, alisema Tume inasikitishwa kuona baadhi ya vyama kutumia majukwaa vibaya.
Alisema kipindi kilichobaki kuelekea uchaguzi mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani ni fursa ya kipekee kwa wagombea kujinadi kwa sera nzuri ambazo zitawavutia wananchi.
“Ni fursa ya kipekee kwa viongozi wa siasa hapa Tanga kukutana hapa na kujadili mambo ya msingi kuelekea uchaguzi----natambua wengi  wenu hapa ni wagombea au wakikilishi wa wawagombea” alisema Mchanga na kuongeza
“Tume inasikitishwa na mwenendo wa kampeni majukwaani ----baadhi ya vyama vimekuwa vikitoa maneno yasiyo mazuri kwa washindani----hebu zitumieni siku hizi chache zilizobaki kutoa sera zitakazowavutia wapiga kura” alisema
Mchanga amewataka wagombea pamoja na wanasiasa kuyatumia majukwaa yao kuzungumzia suala zima la amani pamoja na kunadi sera zao kwa wananchi ili kuweza kuwavutia na kuvuna wapiga kura.
Kwa upande wake Mgombea Udiwani kata ya Mwanzange, Rashid Jumbe wa Chama Cha Wananchi (CUF) ameitaka tume hiyo kusimamia uchaguzi kwa haki na amani bila ushabiki wa chama chochote.
Alisema vipindi vya uchaguzi  Tume ya Uchaguzi imekuwa ikilalamikiwa katika mchakato mzima wa uchaguzi na hivyo kuitaka tuhuma hizo kuzifuta na badala yake kusimamia kwa haki .
“Mheshimiwa kamishna wa tume ya uchaguzi taifa kwa heshima na taadhima naiomba tume yako kusimamia kwa haki uchaguzi huu kwani tumezoea kuona uvurugwaji kuanzia upigaji kura hadi uhesabuji na utangazaji” alisema Rashid na kuongeza
“Hapa kwetu hakuna dalili za viashiria vya fujo wala zogo----ila natoa angalizo simamieni uchaguzi ili uwe huru na haki kwa kila chama kinachoshiriki uchaguzi kiridhike” alisema
Alisema uchaguzi wa mwaka huu ni wa ushindani mkubwa kuliko chaguzi zote zilizopita hivyo kuitaka tume hiyo kusimamia kwa haki  bila upendeleo wa chama kimoja .
                                                  Mwisho


 Kamishna wa Chama Cha NCCR Mageuzi Mkoa wa Tanga, Ramadhani Manyeko, akichangia wakati wa mdahalo wa viongozi wa vyama vya siasa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi uliofanyika leo ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.

 Mgombea Udiwani kata ya Mwanzange kupitia CUF, Rashid Jumbe, akichangia wakati wa kongamano la viongozi wa vyama vya siasa na Tume ya Taifa ya  Uchaguzi lililofanyika leo ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.



 Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mjaka Mchanga akifungua kongamano la viongozi wa vyma vya siasa leo ikiwa ni kuelekea uchaguzi mkuu


No comments:

Post a Comment