Saturday, October 31, 2015

WATU ZAIDI YA 200 WADAIWA KUPOTEZA MAISHA BAADA YA NDEGE KUANGUKA,EGYPT

Ndege imeanguka Egypt na watu zaidi ya 200… chanzo? vifo? hiki ndio kilichonifikia

Ajali za ndege huwa ni chache sana ukiinganisha na ajali za usafiri mwingine kama magari na meli, hiyo sina imefanya usafiri wa ndege kupewa namba moja ya usafiri salama zaidi Duniani kwa muda mrefu !!
Ndege ya abiria iliyokuwa inamilikiwa na Russia imeripotiwa kupata ajali saa chache zilizopita, kulikuwa na ripoti tofauti kuhusu usalama wa abiria 224 ambao walikuwa ndani ya Ndege hiyo lakini Ubalozi wa Russia uliopo Egypt wamethibitisha vifo vya wato wotw waliokuwa ndani ya ndege hiyo.
Plane Crush
Kati ya watu hao waliokuwemo, 217 ni raia wa Russia, pamoja na wafanyakazi saba ambao walikuwa wakihudumia ndani ya ndege.
Ndege hiyo ilitoka Egypt ikielekea St. Petersburg, Russia… ndege ilipotea kuonekana kwenye rada na muda mfupi baadae ikaanguka eneo la Sinai.

No comments:

Post a Comment