Thursday, October 22, 2015

MGOMBEA UDIWANI KATA YA VUGA BUMBULI ADAI KUJENGA KIWANDA CHA KUSINDIKA MATUNDA



Tangakumekuchablog
Bumbuli, MGOMBEA Udiwani kata ya Vuga jimbo la Bumbuli Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, Dhahabu Jumaa kupitia CCM, amesema endapo atachaguliwa kuwa Diwani atahakikisha kero ya maji inapatiwa ufumbuzi sambamba na kiwanda cha kusindika matunda..
Akizungumza katika mkutano wa kuomba kura leo kijiji cha Vuga juu, Dhahabu, alisema anatambua kero za wananchi wa kata hiyo hivyo kuwaomba kumchagua kwa kura nyingi ili kuwatatulia na kudai kuwa muarobaini wa kero hizo yuko nazo.
Alisema hakuna sababu ya wakulima kuwa masikini na kuwa mitaji kwa matajiri na badala yake atawashirikisha wafadhili na wawekezaji wa ndani na nje  kujenga kiwanda cha kusindika matunda ndani ya kata hiyo inayongoza kwa kilimo cha mbogamboga na matunda .
‘Ndugu zangu mimi ni kijana wenu mdogo mtiifu nisie na makuu si kwa kijana wala mzee----kwa maana hiyo nawaomba munichague kwa kura nyingi kuwa diwani wenu” alisema  Dhahabu na kuongeza
“Muarobaini wa soko la kuuzia mazao yenu pamoja na kiwanda cha kusindika matunda ni mimi Dhahabu----si munaliona jina langu liko juu zaidi ya lulu na almasi” alisema
Alisema kwa kutumia uzoefu wake na mahusiano mazuri na viongozi na wafadhili wan je atahakikisha kiwanda cha kusindika matunda kinajengwa ndani ya kata hiyo ambayo amedai kuwa ndio inayongoza kwa kilimo cha mbogamboga.
Akizungumzia kuhusu barabara , mgombea huyo alisema atatengeneza miundombinu ya kuwawezesha wakulima mashambani wanayafikia masoko kwa urahisi hata nyakati za mvua.
Alisema kwa sasa njia nyingi zimekuwa kero kutoa mazao mashambani kutokana na mvua zinazonyesha na njia kusababisha matope na magari kukwama  na hivyo kusema kuwa atazichonga ili ziweze kupitia nyakati zote za mvua na jua.
“Mukinichagua kuwa diwani wenu kero ya wakulima kutoa mazao yao mashambani nyakati za mvua zitaisha----nitazichonga ili kupitika nyakati zote iwe mvua au jua” alisema Dhahabu
Aliwataka wananchi wa kata hiyo kujitokeza kwa wingi siku ya upigaji kura na kumchagua kwa kura nyingi ili  kuwa Diwani wao  na kuweza kuwaletea maendeleo na kudai kuwa ofisi yake muda wote itakuwa wazi kupokea kero za wananchi.
                                                  Mwisho

No comments:

Post a Comment