Friday, October 23, 2015

MUSSA MBAROUK ADAI AHADI ZOTE ALIZOZITOA ATAZITEKELEZA



Tangakumekuchablog
Tanga, MGOMBEA Ubunge jimbo la Tanga mjini, Mussa Mbarouk (CUF) amewataka wananchi kumpa ridhaa ya kuwa Mbunge wao na kusema kuwa ahadi zote alizozitoa atazitekeleza kwani yuko na uwezo nao.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kuomba kura leo barabara ya 13 Ngamiani kati, Mussa aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kumchagua kuwa Mbunge wao ili kuufufua uchumi wa Tanga.
Alisema baada ya kufa kwa viwanda uchumi wa Tanga umekufa na kusababisha wafanyabiashara na wawekezaji kuukimbia mji huo na hivyo kuwataka wananchi kumchagua ili kuweza kuirejesha Tanga katika ramani yake katika uchumi.
“Ndugu zangu wananchi wa Tanga nawaombeni sasa sana musije fanya makosa kwa kumchagua mwengine asie kuwa mimi---kila mtu ni shahidi seheme zote za viwanda sasa ni magofu na maficho ya vibaka” alisema Mussa na kuongeza
“Ahadi zangu nilizozitoa mwanzo wa kampeni zangu hadi hii leo ni za ukweli na niko na uwezo ndio nikazitangaza----ili munipime na kunisuta jaribuni kunipa ubunge  na kuona” alisema
Nae mgombea Udiwani kata ya Ngamiani kati kupitia CUF, Habib Mpa, alisema safari hii CCM imekabwa pabaya na hivyo haiwezi kufurukuta havyo wananchi kutegemea ushindi wa mwaka.
Alisema Chama hicho kimefikia kikomo cha kuongoza hivyo kutakiwa kuwekwa kwanzo na kuweza kujipanga upya na kusubiri mwaka 2020 endapo kitakuwepo na kuingia ulingoni.
“Wananchi wenzangu tuwe na utulivu  mara baada ya kupiga ili CCM wasije kusema sisi tumefanya fujo kwani wameshajitambua kuwa hapa hawana chao” alisema Mpa
Alisema CUF iko na uhakika wa kulinyakua jimbo hilo hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kila mmoja aliejiandikisha kuhakikisha atapiga kura na kumchagua Lowassa, Mussa na Habib Mpa ili kuweza kutengeneza timu ya maendeleo.
                                                         Mwisho

No comments:

Post a Comment