Saturday, October 31, 2015

CHALSEA BADO YAENDELEZA UTEJA UINGEREZA

Full Time ya Chelsea Vs Liverpool

Ligi Kuu soka Uingereza imeendelea tena October 31, kwa michezo kadhaa kupigwa wakati klabu ya Chelsea ya Uingereza iliyochini ya kocha wa kireno Jose Mourinho iliwakaribisha majogoo wa jiji Liverpool katika dimba la Stamford Bridge kucheza mechi yake ya 11 katika Ligi.
P151031-027-Chelsea_Liverpool-1200x806
Chelsea iliingia uwanjani ikiwa na presha ya rekodi mbovu ambayo imetokana na kutokufanya vizuri katika mechi zake kumi za mwanzo kwani ilikuwa imeshinda mechi tatu, sare mechi mbili na kufungwa mechi tano, hiki ni kipindi kigumu kwa Chelsea ambayo ni Bingwa mtetezi wa Ligi hiyo licha ya kuwa yupo katika nafasi za chini katika msimamo wa Ligi.
Football - Chelsea v Liverpool - Barclays Premier League - Stamford Bridge - 31/10/15 Ramires celebrates after scoring the first goal for Chelsea Action Images via Reuters / John Sibley Livepic EDITORIAL USE ONLY. No use with unauthorized audio, video, data, fixture lists, club/league logos or "live" services. Online in-match use limited to 45 images, no video emulation. No use in betting, games or single club/league/player publications. Please contact your account representative for further details.
Hata hivyo mechi imemalizika kwa klabu ya Chelsea kukubali kupokea kipigo cha goli 3-1 na kuendelea kuweka mashakani kibarua cha kocha wao Jose Mourinho. Magoli ya Liverpool yalifungwa na Philippe Coutinho dakika ya 45 na 74 huku Christian Benteke akikamilisha goli la tatu dakika ya 83, Chelsea walipata goli la kufutia machozi dakika ya 4 ya mchezo kupitia kwa Ramires.

No comments:

Post a Comment