Thursday, October 22, 2015

WASHABIKI WA MAN CITY YAINGIZA MATATIZONI

Baada ya mashabiki wa Man City kuzomea wimbo wa UEFA, klabu yao kukumbana na adhabu hii…

Klabu ya Manchester City ya Uingereza ambayo usiku wa October 21 ilicheza mechi dhidi ya klabu ya Sevilla katika uwanja wake wa nyumbani wa Etihad. Kabla ya kuanza kwa mchezo huo ambao klabu ya Manchester City iliibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Sevilla kuna tukio lilijitokeza ambalo huenda litaigharimu Man City.
Usiku wa mechi hiyo kabla ya kuanza kwa mchezo wakati wimbo wa UEFA unaimbwa mashabiki wa klabu ya Man City walizomea wimbo huo, hivyo  tukio hilo lazima Man City watapigwa faini kutoka kwa shirikisho la soka barani Ulaya. Man City inatajwa kupigwa faini ila bado haijajulikana kama itatozwa kiwango cha kawaida au zaidi.
Video ya mashabiki wakizomea wakati wa wimbo huo.

Mashabiki hao walizomea wakati wa wimbo huo kutokana na UEFA kuingiza kipengele cha Financial Fair Play penalties (FFP) kwa mwaka uliyopita kitu ambacho mashabiki hao hawakubaliani nacho. Mashabiki hao wanaamini UEFA wanataka kuitoa klabu yao katika muundo wa kiundeshaji wa kisomi.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment