Monday, October 19, 2015

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA TANGA MJINI CUF KUREJESHA JIJI LA TANGA MAHADHI YAKE



Tangakumekuchablog
Tanga,MGOMBEA Ubunge jimbo la Tanga mjini, Mussa Mbarouk (CUF) amesema endapo atachaguliwa kuwa Mbunge atahakikisha  taa za barabarani zinawaka  usiku ili kuwawezesha wafanyabiashara shughuli zao  hadi usiku na kuongeza kipato chao.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni jan barabara ya 15 kata ya Majengo, Mussa alisema jiji la Tanga limepoteza hadhi yake kutokana na kutokuwa na taa za barabarani na kusababisha giza nyakati za usiku.
Alisema awali jiji hilo lilikuwa likipendezeshwa na taa za barabarani nyakati za usiku jambo ambalo lilikuwa likiwawezesha wajasiriamali wanawake na wanaume kufanya biashara zao za kuuza samaki na maandazi na kupunguza umasikini majumbani.
“Ndugu zangu wananchi wa jimbo la Tanga nawaomba musifanye mchezo katika kuchagua viongozi ambao watawatatulia kero zenu zaidi ya viongozi wa ukawa----nichagueni mimi kwani uwezo wa kuongoza niko nao” alisema na kuongeza
“Mukinichagua nitalirejesha jiji letu katika muonekano kama wa zamani mataa yote barabarani yatawaka na kuwa kama majiji mengine nyakati za usiku-----taa zipo sijui kwa nini haziwashwi---nasema mimi nitaziwasha” alisema Mussa
Kwa upande wake mgombea Udiwani  kata ya Majengo, Suleiman Idd, alisema endapo atachaguliwa kuwa Diwani, atahakikisha kodi ya usafi wa mazingira unaondoshwa pamoja na kodi za leseni za biashara ndogondogo ikiwemo uuzaji wa kahawa na biashara za mikononi.
Alisema kodi hizo zimekuwa kero kwa wafanyabiashara wadogowandogo wa kuuza kahawa barabarani pamoja na karanga  hivyo kuwataka wananchi kumchagua kwa kura nyingi.
“Ndugu zangu mimi ni kijana wenu mtiifu na kila mmoja hapa ananitambua utendaji wangu ----- sina shaka mutanichagua kwa kura nyingi na nitawalipa fadhila kwa kuwaondolea kodi za kupandikiza” alisema Idd
Alisema atasimamia maendeleo ya kata yake kwa kuhakikisha usafi wa mazingira na wafanyabiashara hawasumbuliwi na askari mgambo katika kazi zao za kujipatia kipato.
                                           Mwisho

No comments:

Post a Comment