Friday, October 23, 2015

DANIEL STURRDGE BADO MAJERUHI

Daniel Sturridge atacheza katika mechi dhidi ya Southampton? haya ndio majibu ya Jurgen Klopp


Kocha wa klabu ya Liverpool ya Uingereza Jurgen Klopp ambaye amejiunga na Liverpool wiki kadhaa zilizopita kukifundisha kikosi hicho cha Anfield amethibitisha maendeleo ya hali ya Daniel Sturridge kuhusu tatizo la goti lake alilolipata wakati wa mazoezi wiki iliyopita.
Jurgen Klopp amethibitisha kuwa huenda mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza akacheza katika mechi yao ya Jumapili dhidi ya Southampton, mchezo ambao utachezwa katika uwanja wa nyumbani wa Liverpool Anfield. Klopp amesema kucheza kwa Daniel Sturridge kunategemeana na hali yake ya kila siku .
“Nimezungumza na Sturridge hali yake sio nzuri sana kwa majeruhi aliynayo tunatakiwa kumuangalia siku baada ya siku. Kwa mfano kama ataweza kufanya mazoezi vizuri kesho tutakuwa na maamuzi ya kuchagua kama acheze au la kwa sababu jeraha lake sio kubwa sana”>>> Jurgen Klopp
2DAD30A000000578-0-Klopp_replaced_Rodgers_at_Liverpool_after_the_Northern_Irishman_-a-57_1445595609144
Daniel Sturridge alipata majeraha ya goti wiki iliyopita wakati akiwa mazoezini baada ya kugongana kwa bahati mbaya na Jordon Ibe, jeraha ambalo lilichangia kukosa mechi ya Europa Ligi kati ya Liverpool dhidi ya Rubin Kazan iliyochezwa usiku wa October 22, taarifa rasmi za kucheza au kutocheza katika mechi dhidi ya Southampton kutategemeana na maendeleo yake.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment