Monday, October 26, 2015

KITANDULA AIBUKA TENA KIDEDEA,MKINGA



Tangakumekuchablog
Mkinga,MSIMAMIZI wa Uchaguzi jimbo la Mkinga ambaye pia ndie Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya, Amina Mohammed Kiwanuka, amemtangaza, Dustan Kitandula kupitia CCM kuwa ndie mshindi wa jimbo hilo.
Akimtangaza mgombea huyo ambaye aliwashinda wagombea watatu, Ali Pendeza Mwita wa ACT- Wazalendo, Recho Sadick wa Chadema, Bakari Kassimu wa Chama cha Wananchi CUF
Alisema Kitandula amepata kura 21,623 sawa na asilimia 54.192 ambapo Bakari Kassim wa CUF amepata kura 13,547 sawa na asilimia 34.43 na Recho Sadick wa Chadema amepata kura 3,789 sawa na asilia 9.63 na Ali Pendeza aliepata kura 402 sawa na silimia 1 .
Alisema kwa matokeo hayo anamtangaza Dustan Kitandula  wa CCM kuwa Mbunge wa jimbo hilo kwa miaka mitano.
                                       Mwisho

No comments:

Post a Comment