Friday, October 16, 2015

MGOMBEA UDIWANI KATA YA MAJENGO TANGA AJITAPA



Tangakumekuchablog
Tanga,MGOMBEA Udiwani kata ya Majengo Tanga mjini, Nassir Makata (CCM), amesema endapo atachaguliwa atahakikisha barabara zote za vumbi ndani ya kata hiyo zinajengwa kwa kiwango cha lami.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kuomba kura Leo uliofanyika barabara ya 15, Makata alisema maendeleo hayawezi  kuwafikia wananchi bila kuwa na barabara nzuri.
Alisema barabara zote ambazo ni za vumbi na mashimo atahakikisha zinatengezewa kwa kiwango cha lami na hivyo kuwataka wananchi kumchagua kwa kura nyingi ili aweze kuingia katika baraza la madiwani na kuitekeleza ahadi yake hiyo.
“Ndugu zangu wananchi mimi ni kijana wenu mtiifu na hakuna hata mmoja ambaye hanijui mei---nimekulia hapa hapa nimesoma hapaha hata watoto mitaani wananijua” alisema Makata na kuongeza
“Nichagueni mimi niwatengenezee barabara kwa kushirikiana na madiwani wenzangu na Serikali kwani bila nyinyi sitoweza kufanikisha adhma yangu” alisema
Akizungumzia ajira kwa vijana, mgombea huyo alisema ataunda vikundi vya ujasiriamali kwa na kuwapatia mikopo ikiwa na pamoja na masoko ambayo watakuwa na uhakika wa kuuza bidhaa zao.
Alisema vijana wengi wamekuwa hawana shughuli za kufanya wakati kazi ziko nyingi ila nyenzo wanashindwa kupata hivyo kuwaahidi kumchagua na kumaliza kero yao.
“Vijana wenzangu natambua kuwa kero yenu kubwa ni ajira ambayo kwa kipindi kirefu ndio kilio chenu----muarobaini wenu ni mimi kwa kunichagua kwa kura nyingi kuwa mwakilishi wenu” alisema Makata
Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura wake kw waume walemavu na wazee ili kumchagua na kuweza kuwa mwakilishi wao ndani ya kata na kutoa ahadi kuwa kero zao atazishughulikia .
                                                          Mwisho

No comments:

Post a Comment