Thursday, October 22, 2015

LIVAPOOL YATOKA SARE UEFA

Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ilichezwa October 20 na 21 lakini Alhamisi ya October 22 iliendelea michezo ya UEFA Europa Ligi ambayo zamani ilikuwa inafahamika kama Uefa ndogo, October 22 imepigwa michezo hiyo katika muendelezo wa michezo ya hatua ya makundi.
Generated by  IJG JPEG Library
Liverpool ambayo inafundishwa na kocha mpya raia wa kijerumani Jurgen Klopp ambaye aliingia klabuni hapo siku kadhaa nyuma kuchukua nafasi ya Brendan Rodgers, imekubali kutoka sare ya goli 1-1 katika mchezo uliyochezwa katika uwanja wake wa Anfield dhidi ya klabu ya Rubin Kazan.
during the UEFA Europa League Group B match between Liverpool FC and Rubin Kazan at Anfield on October 22, 2015 in Liverpool, United Kingdom.
Liverpool ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani ilikubali kuruhusu goli la mapema lilofungwa na  Marko Devic dakika ya 15, goli ambalo lilidumu hadi dakika ya 37 ambapo Emre Can aliisawazishia Liverpool. Dakika ya 36 Oleg Kuzmin wa Rubin Kazan alionyeshwa kadi ya nyekundu baada ya awali kuonyeshwa kadi ya njano.
during the UEFA Europa League Group B match between Liverpool FC and Rubin Kazan at Anfield on October 22, 2015 in Liverpool, United Kingdom.
Kwa habari,matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment