Saturday, October 31, 2015

CHALSEA YABAGWA , MAN YAAMBULIA SARE


MATOKEO LIGI KUU YA ENGLAND JANA
Crystal Palace 0-0 Manchester United
Swansea City 0-3 Arsenal
West Bromwich 2-3 Leicester City
Newcastle United 0-0 Stoke City
Watford 2-0 West Ham United
Manchester City 2-1 Norwich City
Chelsea 1-3 Liverpool
Leo ; Novemba 1, 2015
Everton Vs Sunderland (Saa 10:30 jioni)
Southampton Vs Bournemouth (Saa 1:00 usiku)
J’tatu Novemba 2, 2015
Tottenham Hotspur Vs Aston Villa (Saa 5:00 usiku)


TIMU ya Arsenal imeendelea ‘kula sahani moja’ na Manchester City kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Swansea City jioni ya jana Uwanja wa Liberty.
Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Olivier Giroud dakika ya 49, Laurent Koscielny dakika ya 68 na Joel Campbell dakika ya 73 na sas Arsenal inafikisha pointi 25 sawa na Man City baada ya timu kucheza mechi 11, ingawa inabaki nafasi ya pili kwa kuzidiwa wastani wa mabao.
Michezo mingine ya ligi hiyo , Crystal Palace imelazimishwa sare ya 0-0 na Manchester United Uwanja wa Selhurst Park sawa na Newcastle United na Stoke City Uwanja wa St. James' Park.
Leicester City imeshinda ugenini 3-2 dhidi ya West Bromwich Albion Uwanja wa The Hawthorns mabao yake yakifungwa na Riyad Mahrez dakika ya 57 na 64 na Jamie Vardy dakika ya 77, wakati ya wenyeji yamefungwa na Salomon Rondon dakika ya 30 na Rickie Lambert kwa penalti dakika ya 84.

Mabao ya Odion Ighalo dakika ya 39 na 48 Uwanja wa Vicarage Road yameipa Watford ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham United, wakati Manchester City imeshinda 2-1 dhidi ya Norwich City Uwanja wa Etihad, mabao yake yakifungwa na Nicolas Otamendi dakika ya 67 na Yaya Toure kwa penalti dakika ya 89, huku la wageni likifungwa na Cameron Jerome dakika ya 83.
Mchezo uliotangulia jioni ya leo, Chelsea imeendelea kuboronga baada ya kufungwa 3-1 nyumbani Uwanja wa Stamford Bridge na Liverpool.

Ramires Santos do Nascimento alianza kuifungia The Blues dakika ya nne, kabla ya Philippe Coutinho kuisawazishia Liverpool dakika ya 48 na kuifungia la pili dakika ya 74, huku la tatu likifungwa na Christian Benteke dakika ya 83.
Winga wa zamani wa Man United, Zaha akijaribu kupasua katikati ya wachezaji wa timu hiyo, Marcos Rojo na Morgan Schneiderlin

No comments:

Post a Comment