Friday, October 23, 2015

KIDEGE NAE, HAACHI TU VITUKO



Tangakumekuchablog
Tanga, KIPINDI hiki cha kampeni cha lala salama katika viwanja vya kampeni hakukosi vituko na kila siku vinatokea vipya na hiki chengine  cha mgombea Ubunge jimbo la Tanga mjini kupitia ACT-Wazalendo, Ahmed Kidege amesema yeye ni Zitto Kabwe wa Tanga na ni jembe la mjini.
Mgombea huyo ambaye kwa siku za hivi karibuni amekuwa kivutio cha wengi kwa kujenga na kutoa hoja ambapo pia hutoa burudani ya baadhi ya sera zake ambapo leo alisema yeye  ni Zitto Kabwe wa Tanga na kusema CCM na Ukawa wataheshimiana Bungeni.
Alisema wakimchagua kuwa Mbunge wao hatakubali kuona ubadhirifu wa pesa za wananchi zikitafunwa ovyo ovyo hivyo yeye na Zitto watakuwa tayari kurusha ngumi Bungeni.
Alisema kama Bunge la Uingereza lilitifuka kwa kupigana iweje Bunge la Tanzania ikibainika kikundi cha watu au mtu mmoja kushindwa kujenga hoja za upotevu wa pesa za wananchi na hapo ndipo watakapomtambua.
“Ndugu zangu wananchi wa jimbo hili la Tanga mjini nadhani munanitambua kuwa mimi ni Zitto Kambwe wa Tanga----pia munanitambua kuwa pia ni jembe la Tanga” alisema Kidege na kuongeza
“Kwa wale ambao walikuwa hawanielewi na hivyo naitumia nafasi hii kwa kuwaeleza kuwa mimi ni Zitto kwabwe-----tukingia Bungeni mutafurahi na kila siku kipindi cha kutoka Bungeni mutaomba dua umeme usizimwe mukakosa uhondo” alisema
Akizungumzia siku ya kupiga kura kesho (keshokutwa) Kidege aliwataka wananchi kila aliejiandikisha kuyatumia masaa yaliyobaki kwa kukitunza kitambulisho chake na kupiga kura October 25.
Alisema masaa hayo yanaweza kutumika vibaya ima kwa kuibiana vitambulisho au kufichiana ikiwa na pamoja na kuviuza kwa wapinzani ambao amedai kuwa maji yako shingoni na wanatapatapa.
Aliwataka ili kuweza kuitumia haki yao ya kupiga aliwataka wananchi kumchagua kuwa Mbunge wao pamoja na kura zote kumpa Anna Mgwira na kuwa Rais wao na kudai kuwa ataufufua uchumi ulioporomoka.
                                                       Mwisho

No comments:

Post a Comment