Sunday, October 18, 2015

PAPA FRANCIS KUWEKA HISTORIA LEO

Papa Francis kuweka historia leo

Historia ya kanisa katoliki inatarajiwa kuandikishwa upya leo na Papa Francis huko Vatican.

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis anatarajiwa kuwatawaza mume na mke kuwa watakatifu.
Louis na Zelie Martin walikuwa wapenzi waloishi katika karne 19.
i Wawili hao  walifanikiwa kuwapata watoto 9, japo wanne waliaga dunia wakiwa bado wachanga.
Watano waliojaliwa kuishi hadi kuwa watu wazima waliishia kuwa watawa wote.
Mdogo zaidi kati yao ndiye aliyepata umaarufu zaidi na alifahamika kwa jina la Theresa kutoka Lisiex.

Theresa alisifiwa kwa maisha yake ya ukristo akitawazwa kuwa mtakatifu mwaka wa 1925.
Shughuli hii ya leo itafanyika katika ukumbi wa kanisa hilo huko Vatican ambapo mkutano wa viongozi wa kidini au makadinali unaendelea.
CHANZO BBC
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment