Tuesday, October 20, 2015

MGOMBEA WA ACT, WAZALENDO ATAJA VIPAUMBELE VINNE



Tangakumekuchablog
Tanga, MGOMBEA Ubunge jimbo la Tanga mjini kupitia ACT-Wazalendo, Ahmed Kidege, amevitaja vipaumbele vyake vinne endapo atachaguliwa kuwa Mbunge kuwa ni  Elimu, Ajira, Afya na Miundombinu na kuwataka wananchi kumuamini.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara mtaa wa Madina kata ya Mikanjuni, Kidege alisema anatambua wananchi shinda zao na hivyo vipaumbele hivyo ni ndio ufumbuzi  wa maisha hivyo kuwataka  kutofanya makosa.
Alisema vijana wengi hawana kazi na wamekuwa wakizurura mitaani  na baadhi yao kujitumbukiza katika matumizi ya madawa ya kulevya na kufanya vitendo vya uporaji na wizi wa mifukoni.
“Ndugu zangu wamepita wagombea wengi kuomba kura kwenu lakini hakuna hata mmoja mweye vipaumbele vitakavyomuondolea umasikini mwananchi----nasema hivi kwa kuamini nina uwezo” alisema Kidege na kuongeza
“Nichagueni mimi Kidege na acheni ushabiki wa vyama ambavyo havina sera wala muelekeo---ushabiki wenu utakuja kuwagharimu na kuja kunikumbuka ni mimi ni mimi Kidege jamani” alisema
Alisema atahakikisha hakuna mtoto atakaeshindwa kwenda shule kwa sababu ya sare au vifaa vya shule hivyo mfuko wa Mbunge utahudumia wanafunzi wa msingi na sekondari.
Alikitaja kipaumbele chengine kuwa ni ajira ambapo atahakikisha hakuna kijana anaezurura mitaani kwa kukosa kazi ya kufanya na hivyo atanzisha miradi ya ujasiriamali kwa kuanzisha vikundi vya vijana.
Kipaumbele kingine alikitaja kuwa ni afya ambapo atatenga vitengo maalumu kwa wanawake na wanaume pamoja na wazee kwa kudai kuwa ni kuondosha kero ya misongomano wakati wa kuhitaji matibabu.
Alisema katika vituo vya afya na zahanati amedai kuwa hakuna utaratibu wa kijana, mzee wala mtoto hivyo na kusababisha kero na kutojulikana mgonjwa wala mzima.
Mgombea huyo wa Ubunge alikitaja kipaumbele cha nne kuwa ni miundombinu na kusema kuwa atahakikisha barabara zote za mjini zinakuwa katika kiwango cha lami na zile za nje ya jiji ataziweka vifusi ziweze kupitika na kuwawezesha wakulima kupeleka mazao yao katika masoko.
Aliwataka wananchi wa jimbo hilo kumchagua kwa kura nyingi na kuacha ushabiki wa vyama kwa madai kuwa yuko na uzoefu wa kuongona kiutawala hivyo Mbunge anaefaa ni yeye tu.
                                              Mwisho

No comments:

Post a Comment