Monday, October 26, 2015

HATMA YA JOSE MORINHO YAINGIA SURA MPYA

Hatma ya Jose Mourinho Chelsea imeingia katika headlines ya magazeti ya Uingereza October 26

Bado mashabiki na wapenzi wa soka duniani kote wanajadili juu ya mwenendo wa klabu ya Chelsea kama Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Uingereza. Chelsea ambayo inafundishwa na Jose Mourinho kwa awamu ya pili sasa imekuwa haipati matokeo mazuri kwa siku za hivi karibuni na kwa sasa ipo nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi huku ikiwa na point 11.
Kufuatia mwenendo mbovu wa timu hiyo stori kutoka katika magazeti ya Uingereza ya leo October 26 yanaeleza kuwa mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich huenda akamfuta kazi Jose Mourinho kwa mara ya pili kama timu ya Chelsea ambayo itacheza mechi na Liverpool katika uwanja wake wa nyumbani Jumamosi ya October 31 itafungwa.
Mourinho-Lampard-City-513573
Taarifa kutoka katika vyombo vingi vya habari Uingereza zinasema kama Chelsea itafungwa na Liverpool Stamford Bridge basi mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich atamfuta kazi Jose Mourinho, kama Mourinho akifukuzwa Chelsea itakuwa ni mara ya pili kufukuzwa kazi baada ya kufukuzwa kwa mara ya kwanza 2007 na kurejea 2013. Nafasi ya Mourinho Chelsea inatajwa kuchukuliwa na Carlo Ancelotti au Guus Hiddink
Kwa habari, matukuio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment