Tuesday, October 20, 2015

OSCAR KUTUMIKIA KIFUNGO CHA NYUMBANI SASA

Oscar Pistorius kwenye headlines, sasa kutumikia kifungo cha nyumbani!

Mwanariadha maarufu kutoka South Africa Oscar Pistorius, aliingia kwenye headlines baada ya kesi ya yeye kumpiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp siku ya wapendanao mwaka 2013 kushika uzito mkubwa nchini South Africa… kesi ikaenda Mahakamani na Oscar akasema hakudhamiria kufanya vile, ilikuwa ni bahati mbaya kwani aliamini kuwa waliingiliwa na mwizi nyumbani kwao… mwisho wa siku Mahakama ikaamua  kumpatia Oscar adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela!
Oscar Pistorius, gestures, at the end of the fourth day of sentencing proceedings in the high court in Pretoria, South Africa, Thursday, Oct. 16, 2014. Following the testimony hearing, which is expected to end this week, Judge Thokozile Masipa will rule on what punishment Pistorius must serve after convicting him of culpable homicide for shooting his girlfriend Reeva Steenkamp through a toilet door in his home.(AP Photo/Alon Skuy, Pool)
Oscar Pistorius
Mwaka jana Mahakama ilisema kuwa kitendo alichokifanya Oscar Pistorius kilikuwa ni uzembe” lakini hakiashirii mauaji wala hakikuonyesha dhamira ya kuchukua maisha ya mpenzi wake… Hiyo ilikuwa ni October mwaka 2014 na kipindi chote hicho Oscar alikuwa jela.
Headlines zilibadilika siku ya jumatatu baada ya vyombo vya habari kutangaza kuwa Oscar Pistorius atatolewa jela na kuwekwa chini ya ulinzi kwa kutumikia kifungo cha nyumbani baada ya Bodi ya Parole nchini South Africa kupitisha kifungo hicho kwa miaka minne.
OSCAR5
Leo vyombo vya habari vimeripoti kuwa Oscar ametolewa jela na ataanza kutumikia kifungo chake cha nyumbani kwa mjomba wake jijini Pretoria, South Africa na Sheria za South Africa hazimruhusu Oscar Pistorius kufanya chochote mpaka kifungo chake kitakapoisha ila atatakiwa kufanya kazi za kijamii ikiwa ni sehemu ya vigezo alivyowekewa na Bodi ya Parole ya South Africa.
OSCAR4
Wanasheria wa Serikali wameanza maandalizi ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi hayo ya Mahakama kwa kuamini kuwa Oscar Pistorius ambaye ana miaka 28 sasa, anatakiwa ahukumiwe kwa kosa la mauaji… Rufaa hiyo inategemewa kusikilizwa mwezi ujao.
Unaweza pia ukatazama video hii hapa chini kwa taarifa zaidi.

Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment