Wednesday, October 21, 2015

VITUKO KAMPENI, JAMANI WAGOMBEA SASA MUMEZIDI



Tangakumekuchablog
Tanga, KIPINDI hiki cha kampeni za lala salama ukienda katika mikutano huachi kusikia vituko ambavyo vyengine hata hudhanii kuvisikia katika majukwaa ya kisiasa kama hii ya mgombea Ubunge jimbo la Tanga mjini kupitia ACT-Wazalendo Ahmed Kidege.
Jamaa aliwavunja mbavu washabiki na wapenzi wa chama hicho pale aliposema kuwa yuko na taarifa za Ukawa na CCM kuwa wanamroga ili asiupate Ubunge lakini akawambia kuwa jina la Kidege halirogeki hata wakienda chini ya bahari.
Alitoa kali hiyo juzi  wakati wa mkutano wake wa Ubunge kuomba kura kata ya Mikanjuni  mtaa wa Madina na kusema kuwa Ukawa na CCM wakataka wasitake yeye ndie atakekuwa Mbunge wa jimbo la Tanga mjini kupitia ACT, Wazalendo.
“Ninazo taarifa za vyama viwili kuniroga mimi Kidege eti ili niukose ubunge----nawambia jina la Kidege halirogeki si usiku wala mchana na hata waende baharini mimi ndie kidege original” alisema Kidege na kuongeza
“Wanatambua kuwa jimbo la Tanga mjini mwaka huu linatuwa kwa ACT- Wazalendo na ndio maana wamekata tamaa----kama ni kuroga wamroge Kidege mwengine lakini sio mimi sirogeki” alisema
Mgombea huyo aliamsha tena shangwe pale aliposema kuwa CCM mwaka huu iko ICU na matumaini ya kutoka katika chumba hicho salama ni vigumu hivyo wananchi wategemee mabadiliko ya kweli.
Alisema CCM imeshikwa pabaya na tena haina mashiko ya kushika hivyo kilichobaki ni kuporomoka na kuanguka pwaa na kuwataka wananchi kusubiri mabadiliko na kuwataka kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura.
Aliwataka wananchi kumchagua kwa kura nyingi ili kuwa Mbunge wao na kuweza kuwaletea maendeleo ya kweli kwani uwezo wa kuongoza yuko nao hivyo kuwataka kumuamini nae kujiaminisha.
Alisema ahadi zote ambazo amekuwa akizitoa katika majukwaa ya kuomba kura atazitekeleza ikiwa na pamoja na kuboresha elimu, afya , mazingira na miundombinu ya barabara.
                                                     Mwisho

No comments:

Post a Comment