Saturday, October 31, 2015

MABOMU YARINDIMA MKWAKWANI


Penalti iliyofungwa na Raphael Alpha imezua tafrani kubwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga wakati wa mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara.

Kiungo huyo wa Mbeya City alifunga penati hiyo ya dakika ya 90 baada ya Coastal Union kuongoza kwa muda wote.
Hali hiyo ilifanya mashabiki wa Coastal Union kufanya vurugu kubwa ikiwa ni pamoja na kuharibu ubao wa kubadilishia wachezaji, pia ripoti za mwamuzi wa akiba.
 
Polisi walilazimika kuingiza gari katikati ya uwanja na kupambana na mashabiki hao kwa kupiga mabomu ya machozi.

Mashabiki hao waliendelea kurusha mawe wakiwapiga waamuzi ambao walipewa ngao ya Polisi kujilinda wakiwa katika gari la Polisi.







No comments:

Post a Comment