Wednesday, November 16, 2016

AJICHIMBIA KABURI KABLA HAJAFA

Babu wa miaka 89 ajichimbia kaburi Canada

Mzee wa umri wa miaka 89 nchini Canada amegongwa vichwa vya habari nchini humo baada yake kujichimbia kaburi.
Mzee huyo bado yuko buheri wa afya.
"Huwa napenda kuchimba," Jimmy Kickham, kutoka kisiwa cha Prince Edward Island, aliambia CBC News.
Ameongeza kwamba anajivunia kukamilisha mradi huo wake wa kibinafsi.
 Kickham, ambaye anamiliki kazi ya ujenzi, amekuwa akichimba makaburi ya wengine pamoja na mitaro kwa zaidi ya miaka 60.
Kaburi la Bw Kickham Afisa wa makaburi asijiliza Bw Kickham akifafanua ni kwa nini ameamua kuchimba kaburi lake

No comments:

Post a Comment