Sunday, November 27, 2016

ARSENAL IMEFANYA KWELI, YANYAKUA POINT TATU MUHIMU

Ushindi wa Arsenal dhidi ya AFC Bournemouth jana  November 27 2016

November 27 2016  jana klabu ya Arsenal iliikaribisha klabu ya AFC Bournemouth katika uwanja wake wa Emirates kucheza mchezo wao 13 wa Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017.
Katika mchezo huo Arsenal wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-1, magoli yakitiwa wavuni na Alex Sanchez dakika ya 12 na 90 na Theo Walcott dakika ya 53.
3acc319300000578-3975820-image-a-70_1480259266371
Goli pekee la AFC Bournemouth limefungwa na Callum Wilson  dakika ya 23, kufuatia ushindi huo Arsenal wanafikisha jumla ya point 28 na wapo nafasi ya nne wakati AFC Bournemouth wanabaki na point 15 na wapo nafasi ya 11.

No comments:

Post a Comment