Tangakumekuchablog
Mkinga, WAJASIRIAMALI wanawake Tanga
wametakiwa kulitumia soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kutafuta
masoko na kuacha kutegemea masoko ya ndani ambayo hayawezi kuwatangaza.
Akizungumza
kwenye kongamano la Wajasiriamali Wanawake kijiji cha Gombero Tarafa ya Maramba
juzi, Mratibu wa Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake (Inuka), Devid Msuya, alisema
wajasiriamali wengi hawana uelewa wa soko la pamoja.
Alisema wako
wajasiriamali wa kazi za mikono ambao bidhaa zao ziko na masoko nje ya nchi
lakini kutozitangaza kwao zimekuwa zikishilizia mikononi na kushindwa
kutangazika.
“Soko la
pamoja lipo muda mrefu toka lifunguliwe lakini la kushangaza ni kuwa
wajasiriamali wa ndani hawana uelewa wa kulitumia na badala yake wenzao
wamekuwa wakilitumilia ipasavyo” alisema Msuya na kuongeza
“Hebu
tulichangamkie kwani soko hili ndio la kuzitangaza kazi zetu za mikono na
tukiendeleza kulala wenzetu watahozi hadi masoko yetu ya ndani” alisema
Alisema
kwenye soko hilo la pamoja kuna fursa nyingi za kujiendeleza ikiwemo
kubadilishana uzoefu na mbinu za kibiashara na kuweza kufikia kuwa mjasiriamali
wa Kimataifa.
Kwa upande
wake mjasiriamali wa kutengeza mikeka na ungo, Mwanahawa Mbelwa, alisema kutokuwa
na vikundi imekuwa chanzo cha kazi zao kutojulikana.
Alisema awali
waliunda vikundi na kufa kutokana na
kushindwa kupata mikopo hivyo kuzitaka taasisi za fedha na mashirika kutoa
elimu ya vikundi ili kupata mikopo isiyo na riba.
“Hapa tuko wajasiriamali
tofauti ambao kama tutapatiwa mikopo na
elimu ya ujasiriamali na kuunda vikundi tunaweza kuwa wajasiriamli wakubwa na
kuliteka soko la pamoja” alisema Mbelwa
Aliwataka
wajasiriamali wenzake kuunda vikundi na kuweza kupata mikopo katika taasisi za
fedha ili kuweza kuzifanya kazi kwa weledi na kuweza kuyafikia masoko ndani ya
Jumuiya Afrika Mashariki.
Mwisho
No comments:
Post a Comment