Tangakumekuchablog
Tanga, WAJUMBE 14 wa Kamati ya Mawasiliano
na Ujenzi Baraza la Uwakilishi la Zanzibar
wamesema ujio wa Mradi wa Bomba la Mafuta Tanga litaongeza ajira kwa vijana wakiwemo
Wanzanzibar waishio Tanga.
Wajumbe hao
wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hamza Hassan Juma walitembelea bandari ya Tanga eneo la upakuzi wa shehena
ya mizigo na eneo itakapojengwa bandari mpya ya Mwambani.
Akizungumza
mara baada ya ziara hiyo, Hassan alisema
Serikali ya Zanzibar imejipanga kuimarisha bandari zake ikiwemo ya Wete na
Mkoani Kisiwani Pemba ikiwa ni maandalizi ya ujio wa Bomba la Mafuta.
Akizungumzia
kilio cha wafanyabiashara na wasafiri wa
Pemba na Tanga kwa kutumia usafiri wa baharini, Hassan alisema kero hiyo
Serikali inaitambua na jitihada za kuwa na meli ya uhakika inafanywa.
Alisema kuna
baadhi ya wafanyabiashara wa Pemba ambao walikuwa wakichukua bidhaa Tanga
wamekatisha na baadhi yao mitaji kufa kutokana na kutokuwepo kwa usafiri wa
uhakika wa baharini.
Awali
akizungumza na wajumbe hao wa Baraza la Wawakilishi, Kaimu Meneja wa Badari
Tanga, Henry Arika, alisema mchakato wa mradi wa bomba la mafuta unaenda kwa
kasi na kuwataka wawekezaji kutoka Zanzibar kuja kuwekeza.
Alisema Tanga
ziko fursa nyingi za uwekezaji na yako
maeneo mengi hivyo kupitia ujio wa mradi wa Bomba la mafuta amewataka
wawekezaji wa ndani kuchangamkia.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Henry Arika (katikati) akitoa maelezo kwa wajumbe 14 wa Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar walipotembelea bandari ya Tanga kujifunza
Afisa Mtekelezaji Mkuu Bandari ya Tanga, Donald Kaire, akitoa maelezo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar walipofanya ziara bandari hiyo juzi. Katikati ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Henry Arika.
No comments:
Post a Comment