Tangakumekuchablog
Tanga, UFUNGUZI wa ligi ya Azam Federeshen
Cup iliyozinduliwa leo uwanja wa Mkwakwani Tanga umegubikwa na fujo za
washabiki baada ya timu ya Muheza United kufunga goli la pili lililoipa ushindi
wa pointi tatu.
Ugunguzi huo
wa mashindano uliofunguliwa na Makamo wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania,
Walles Karia na viongozi mbalimbali wa mpira ngazi ya Taifa na Mkoa
ulizikutanisha timu ya Muheza United na Safi Politan kutoka Dar es Salaa.
Timu ya
Muheza iliibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 1 na kuibua shangwe kwa washabiki wa
timu hiyo na kulazimika polisi kuwadhibiti washabiki.
Akizungumza
mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo , kocha wa Safi Polistan, Mussa Rashid,
alisema vijana wake walicheza chini ya kiwango na kuruhusu mabao kurejeshwa kwa
urahisi.
Alisema
kipindi cha kwanza walicheza vizuri na kuonyesha dalili za kuongeza magoli
mengine lakini goli moja wachezaji wake walibweteka na kukubali kurejeshwa kwa
urahisi.
“Wachezaji
wangu walibweteka baada ya kupata goli la kwanza lililoenda hadui kipindi cha
pili, wenzetu kipindi cha pili walikuwa mbogo na kutuchanganya” alisema Rashid
Kwa upande
wake, kocha wa Muheza United, Lukindo Domonic, alisema wenzao waliwabeza na
kuona timu za Tanga ni za kunyakuwa pointi tatu na kuondoka zao.
Alisema
wakati walipoenda katika vyumba vya kupumzika aliwaeleza wachezaji wake wanapaswa
kugangamala kuondosha dhana ya kufanywa uwanja wa Mkwakwani kama shamba la
bibi.
“Niliwaeleza
wakati tuko katika vyumba vya kubadilisha nguo kuwa wanapaswa kukomaa ili
kuondosha aibu mbele ya umati uliojitokeza uwanjani” alisema Lukindo
Alisema kwa
ushindi huo wa ufunguzi umewatia morali na ari ya ushindi katika michezo iliyoko mbele yao na
kuwapongeza vijana wake ambao awali wapinzani waliwabeza.
Mwisho
Makamo wa Rais Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, Walles Karia, akisalimia na wachezaji wa timu ya Muheza United ya Tanga na Sifa Politan kutoka Dar es Salaam wakati wa ufunguzi michuano ya Azam Federetion Cup iliyozinduliwa Mkwakwani leo.
Polisi wa kutuliza Ghasia (FFU) akimdhibiti shabiki aliedhaniwa kuwa ni wa timu ya Muheza United ambaye alikuwa akifanya fujo baada ya timu yake kufunga bao la pili na kutaka kuingia uwanjani wakati wa mchezo ligi ya Azam Federeshen Cup uliofanyika leo uwanja wa Mkwakwani Tanga.
No comments:
Post a Comment