Wednesday, November 9, 2016

MPOMOTA MAARUFU WA NGUMI TANGA AKANUSHA KUPIGANA NA AURORA



Tangakumekuchablog
Tanga, PROMOTA wa Ngumi Maarufu Tanga, Karume Kenge, amekanusha taarifa zilizoenea katika mitandao ya Kijamii kuwa amepigana na Mwenyekiti wa Coastal Union ya Tanga, Ahmed Aurora.
Akizungumza na Tangakumekuchablog, Karume Kenge, alisema Taarifa hizo ni za Uongo na Uzushi ambazo amedai kuwa zinataka kumchafua na Mwenyekiti huyo na uongozi wa Coastal Union na wanachama wake.
Alisema yeye hana ugomvi na Mwenyekiti huyo na wamekuwa na maelewano ndani ya uwanja na nje ya uwanja hivyo kuwataka washabiki wa Coastal Union kuzipuuza taarifa hizo.
Amesema wakati wa mechi ya Coastal Union na Njombe Mji kulitokea hali ya Kiushabiki katika jukwaa la Coastal Union kutofurahishwa na aina ya uchezaji  ya wachezaji wa Coastal baada ya kufungwa goli moja.
Alisema kufuatia washabiki kulalamika timu yao kufungwa goli lililoipa ushindi timu hiyo ya Njombe Mji, washabiki walikuwa wakipiga kelele na wala hakutokea kupigana kama taarifa katika mitandao ya kijamii inavyodai.
Karume Kenge, alisema yuko na maelewano na kiongozi huyo wa Coastal Union na wamekuwa marafiki kwa muda mrefu hivyo taarifa hizo ni zauongo na kutaka kuwagombanisha hivyo kuwataka washabiki wa mpira Tanga kuzipuuza.
                                                   Mwisho

No comments:

Post a Comment