FIFA yamuadhibu Saoud al-Mohannadi
Afisa wa soka
kutoka nchini Qatar, ambao ndiyo wenyeji wa kombe la dunia
linalotarajiwa kufanywa mwaka 2022, amepigwa marufuku katika shughuli
zozote zinazohusiana na mpira wa miguu kwa muda wa mwaka mmoja kwa
kukataa kutoa ushirikiano kama shahidi katika uchunguzi unaoendelea.
Msemaji
wa kamati ya nidhamu ya FIFA ,na shirikisho la soka la kimataifa
walisemema kuwa afisa huyo hakuweza kutoa maelezo ya kutosha kwa hofu
ya kuhatarisha kesi, ofisa huyo Saoud al-Mohannadi, pia alipigwa faini
inayokadiriwa kufikia dola za kimarekani elfu ishirini
No comments:
Post a Comment