Wednesday, November 9, 2016

NEW AGE EDUCATION CENTRE TANGA YAWAZAWADIA ZAWADI WANAFUNZI WAKE

 Wanafunzi wa kidato cha sita kituo cha Elimu Cha New Age Education Centre Tanga, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa kituo hicho, Jerry Stivin mara baada ya Tafrija ya kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho wa mwezi jana.
Kituo hicho maarufu Tanga ambacho hutoa kozi mbalimbali yakiwemo masomo ya Sayansi na Hisabati na masomo ya QT pamoja na Lugha za kigeni .
Kituo ambacho kiko Tanga mkabala na Jengo la Shirika la Umeme Tanzania Tanesco kimekuwa kikipokea wanafunzi mbalimbali shuleni, maofisni na wanaojiendeleza kielimu.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkuu wa kituo, Jerry Stivin amewataka wazazi na walezi kuwabidiisha watoto wao katika elimu na kuwa msaada katika maisha yao ya baadae.

 Wanafunzi wa Pree Form One wakisikiliza nasaha kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha Elimu cha New Age Education Centre Tanga, Jerry Stivin

 Mwanafunzi Aisha Mohammed akipokea zawadi kutoka mwalimu wa kituo hico, Amani Baraza


 Mwalimu wa kituo cha Elimu Cha New Age Education Centre Tanga, Madame Suzy Mrutu, akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa Pre Form One Hamadi Zakaria



Walimu wakituo cha Elimu cha New Age Education Centre Tanga, wakiwa katika moja ya majukumu yao ofisini jana.

No comments:

Post a Comment