Friday, November 18, 2016

MACHO YOTE DUNIANI LEO, OLD TRAFORD

Wenger, Mourinho hapatoshi leo

London, England. Ahadi ya kocha Arsene Wenger kumpa mkono hasimu wake Jose Mourinho leo kwenye Uwanja wa Old Trafford, kikosi dhaifu cha United kinachosaka kuduwaza mashabiki wao pia wale wa  Arsenal ni miongoni mwa matukio ya kimichezo yatakayosimamisha dunia kwa dakika 90.

Matukio mengine ni ligi nyingine kali Ulaya, ambako vumbi litatimka kwenye miji ya Madrid, Dortmund na Milan ambako itajaa upinzani  wa aina yake. Klabu mbili za Madrid, Atletico na Real Madrid zitapimana nguvu kwenye mchezo wa Ligi Kuu, La Liga.

Nchini Ujerumani, vinara Bayern Munich wanakuwa wageni wa Borussia Dortmund, ambayo msimu huu imekuwa yenye matokeo tofauti. Kwenye Ligi Kuu ya Italia, vinara Juventus wanakabiliana uso kwa uso na AC Milan kwenye mchezo mwingine unatarajiwa kuwa wenye upinzani mkali.

No comments:

Post a Comment