Rwanda yanunua ndege ya kipekee Afrika nzima, ni ya pili duniani
Huduma
za usafiri wa ndege zinazidi kushika kasi kwenye mataifa ya Afrika
Mashariki kila siku, Kutoka nchini Rwanda nimeipata hii ya Shirika la
ndege la Rwanda, RwandAir kununua ndege mpya aina ya Boeing 737-800 Next
Gen ambayo inatarajiwa kuongeza ushindani wa safari za anga duniani .
RwandAir
imekuwa kampuni ya kwanza barani Afrika na ya pili duniani kununua ndege
ya aina hiyo ambayo imewekwa vifaa vya kuwezesha abiria kutumia huduma
za intaneti kwa njia ya Wi-Fi.
Ndege hiyo
ina uwezo wa kubeba abiria 154 ilitolewa oda ya kununuliwa na Rwanda
miaka 6 iliyopita, imetua kwenye uwanja wa ndege wa Kigali November 16,
2016 saa 10 usiku.
Waziri wa
uchukuzi wa Rwanda Alexis Nzahabwanimana, amesema ndege hiyo mpya
itawezesha shirika hilo kupanua safari zake barani Asia, Ulaya na
Marekani.
Mwezi September
mwaka huu, Serikali ya Rwanda ilinunua ndege nyingine ambayo ni ya
kwanza Afrika Mashariki aina ya Airbus 330-200, iliyopewa jina
la ‘Ubumwe’ ikiwa na maana ya Umoja.
No comments:
Post a Comment