Tangakumekuchablog
Tanga, NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa, Suleiman Joffo, amewataka wakuu wa Idara na
Watendaji maofisini kufanya kazi na kuacha ufanyaji kazi wa mazoea.
Pia alikemea
baadhi ya wakuu wa Idara kuwapandisha
vyeo wafanyakazi kwa misingi ya urafiki na kuwahamisha watumishi kwa chuki.
Akizungumza
na wakuu wa idara na wafanyakazi wa sekta mbalimbali jijini hapa jana, Joffo
alisema kuna baadhi ya wakuu wa Idara wamekuwa wakizifanya ofisi kama mali zao
hivyo kuwataka kubadilika.
Alisema
malalamiko hayo yamekuwa mengi na Serikali kulaumiwa na kusema yoyote ambaye hatokuwa tayari
kufanya uadilifu kuachia ngazi.
“Serikali
inahuzunika kuona malalamiko ya wananchi yamekuwa yakiongezeka kuwalalamikia
wakuu wa idara maofisini, kila siku nimekuwa nikisema huduma ni haki ya kila
mwananchi” alisema Joffo na kuongeza
“Kama kuna
mtumishi au mkuu wa idara anaona majukumu aliyopewa kwa kuomba mwenyewe
yamemzidi ni bora aacie ngazi mapema kwani fagio likipita litakuw alinasafisha”
alisema
Akizungumzia
pesa za Serikali ilizotoa kwa halmashauri nchini kwa ujenzi wa vyumba vya
madarasa na vyoo, Joffo alisema muda uliowekwa mwishoni mwa December ukipita
bila kukamilisha wakurugenzi watawajibishwa.
Alisema
amebaini baadhi ya halmashauri zimeshindwa kukamilisha agizo hilo la Serikali
kwa kushindwa kimaslahi za pande tatu , Afisa elimu, Afisa manunuzi na Injinia.
“Kuna baadhi
ya halmashauri hadi muda huu nikuweka maji mwaga mchanga hakuna lolote
linaloendelea, tunatambua kuwa ni kugombea maslahi na hili niseme muda
ukimalizika na hakuna kiliochofanyika ni uwajibishwaji” alisema Joffo
Aliwataka
wakuu wa Idara na wafanyakazi wenye dhamana maofisini kuacha kufanyiana majungu
na badala yake kufanya kazi kwa bidii na kuwahudumia wananchi kupata huduma
bora.
Mwisho
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo, akikagua ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 1 . 6 inayojengwa na kampuni ya Hari Singh and Sons kwa ufadhili wa Bank ya Dunia. Barabara hiyo hadi kukamilika kwake itagharimu zaidi ya shilingi bilioni 2.
Injinia wa halmashauri ya jiji la Tanga, Arafati Kaniki, akimsomea taarifa ya ujenzi wa barabara ya Nguvumali hadi Kwaminchi, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jaffo, wakati wa ziara yake Tanga
No comments:
Post a Comment