Wednesday, November 16, 2016

MWILI WA ASKARI ANAEDAIWA KUFA KWA KIPIGO TANGA ASAFIRISHWA KWENDA KWAO


Tangakumekuchablog
Tanga, MWILI wa aliekuwa askari wa kituo kikuu cha Polisi cha Chumbageni Tanga, Elizabert  Stephano, uliekufa kwa kudaiwa kupigwa hadi kufa na mpenzi wake ambaye pia ni askari kitengo cha upelelezi kituo cha Chumbageni umesafirishwa kwenda kwao Kilimanjaro.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa, Devid Mngambugha, alisema polisi inamsaka , Michael Komba ili kumfikisha katika vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazomkabili.
Michael Komba ambaye anadaiwa kuhusika na tukio hilo lilitokea juzi saa 9 usiku eneo la Sahare Tanga ambako ni nyumbani kwa marehemu na kudaiwa kumpiga na kumtekeleza hospitali ya Mkoa ya  Bombo.
Alisema polisi kwa sasa inachunguza kituo hilo ikiwa na pamoja na kumsaka mtuhumiwa ambaye hadi sasa hajatiwa nguvuni na kuahidi kumkamata na kuweza kumfikisa mahakamani.
“Kwa sasa ninachoweza kusema kuwa mwili wa marehemu umeshasafirishwa kwenda kwao Kilimanjaro kwa taratibu za kifamilia, na umehifadhiwa hospitali ya KMC” alisema Mngambugha na kuongeza
“Kwa upande wetu polisi tunamsaka ili kumhoji tuhuma zinazomkabili kisha kumpeleka mahakani kujibu tuhuma zinazomkabili” alisema
Baadhi ya majirani kwa marehemu Sahare walidai kuwa wawili hao walikuwa katika ugomvi wa kimapenzi  kila mmoja kumtuhumu mwenzake kumuendea kinyume.
Alidai kuwa walisikia kelele za Elizabert  kuomba msaada na wakati majirani  wakitoka waliwaona wenza hao wakiwa wameondoka na gari na kutokua walikokwenda.
                                                 Mwisho

No comments:

Post a Comment