NATO yamuonya Trump kuhusu uamuzi dhidi yake
Katibu mkuu wa NATO
Jens Stoltennburg amemuonya rais mteule wa Marekani Donald Trump dhidi
ya kufanya maamuzi ya kipekee ,akisema kuwa sio chaguo la muungano wa
Ulaya ama hata Marekani.
Amesema kuwa mataifa ya magharibi yalikabiliwa na changomoto yake kuu ya kiusalama.Wakati wa kampeni zake za uchaguzi bwana Trump aliutaja muungano huo wa kijeshi wa mataifa ya Magahribi kama uliopitwa na wakati.
Alisema kuwa Marekani itafikiri mara mbili kumsaidia mwanachama yeyote wa muungano huo ambaye ameshambuliwa iwapo hajalipa kodi yake ya uanachama.
BBC
No comments:
Post a Comment