Saturday, November 12, 2016

MNARA WAKUMBUKUMBU WA ASKARI WALIOUWAWA TANGA WAKATI WA VITA YA KWANZA YA DUNIA WAZINDULIWA

 BALOZI wa Uingereza nchini, Sarah Cooke, akikata utepe kuzindua mnara wenye majina ya Askari kutoka Mataifa mbalimbali yakiwemo Uingereza, Ujerumani, India na Canada waliouwawa Tanga  wakati wa vita ya kwanza ya Dunia, kulia ni Balozi wa India nchini , Sandeep Arya.
Mnara huo ambao unasimamiwa na Tume ya Jumuiya ya Madola uko na majina 332 .




 Balozi wa India, Sandeep Arya akizungumza wakati wa uzinduzi wa mnara wa askari waliouwawa wakati wa vita ya kwanza ya Dunia Tanga
 Kiongozi wa kidini kutoka dhehebu la Sing Nagi, Sikh Mohan, akiongoza sala ya kuwaombea askari waliouwawa Tanga wakati wa vita ya kwanza ya Dunia ambapo jumla ya askari 332 waliuwawa Tanga.
 Kiongozi wa Shia akiongoza sala ya kuwaombea askari waliouwawa wakati wa vita ya kwanza ya Dunia Tanga


 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Zena Said wa kwanza kushoto akimuonyesha jambo Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke mara baada ya uzinduzi wa mnara wenye majina ya askari 332 waliouwawa  Tanga wakati wa vita ya kwanza ya Dunia, kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Tanga, Daudi Mayeji.
 Askari wa Uingerza na askari wa India wakiteta jambo mara baada ya uzinduzi wa mnara wa askari waliouwawa Tanga wakati wa vita ya kwanza ya Dunia ambapo jumla ya askari 332 waliuwawa Tanga, Majina hayo yamezinduliwa na Tume ya Jumuiya ya Madola

 Viongozi mbalimbali wa kitaifa na Kimataifa walihudhuria uzinduzi huo wa mnara wa majina ya askari waliouwawa Tanga wakati wa vita ya kwanza ya Dunia.




 Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Sekondari na msingi wakiweka mauwa chini ya mnara wa askari waliouwawa wakati wa vita ya kwanza ya Dunia Tanga, Mnara huo ulizinduliwa na Tume ya Jumuiya ya Madola .






No comments:

Post a Comment