HADITHI
YAMENIKUTA SALMA MIE
ILIPOISHIA
Alipotoka nilikwenda kumchungulia kwa dirishani nikamuona
anaelekea kwenye kituo cha daladala. Nikaendelea kumtazama mpaka alipokata
kona.
Bila shaka walishapigiana simu na Chinga tangu akiwa chumbani. Na
alimwaambia kuwa nimemjibu jeuri ndipo akapanga safari ya kwenda kwa dada yake.
Nikawaza.
Niliacha kufagia nikaenda chumbani na kuchukua simu yangu. Na mimi
nikampigia Chinga. Nilipiga kwa muda mrefu lakini Chinga hakupokea simu yangu. Jambo
hilo lilinihuzunisha sana. Ikabidi nijiulize tena iwapo kweli
Chinga bado alikuwa na dhamiri ya kuendelea na mimi.
Kutokana na dukuduku lililonipata sikutoka tena kuendelea kufanya
usafi wa nyumba. Nikajilaza kitandani na kuendelea kuwaza.
Sikutoka mle chumbani hadi ilipotimu saa sita mchana. Nilikwenda
kuchukua soda kwenye friji nikanywa na keki nilizokuwa nimeziweka jikoni kisha
nikaenda kuoga.
Niliporudi nilimpigia simu tena Chinga lakini sasa simu yake ikawa
haipatikani.Nilizidi kuumia moyo wangu na kujuta kumkubali Chinga.
SASA ENDELEA
Nilikaaa mle chumbani hadi jioni nikimsubiri Chinga arudi ili
nijue moja, lakini hadi inafika saa nne usiku si Chinga wala Vicky aliyetokea.
Kwa vile sikuwa nimekula mchana kutwa, nilitoka nikaenda kununua chipsi
na mishikaki nikala na soda. Nilipomaliza kula nilifunga mlango na kwenda
kulala.
Asubuhi kulipokucha niliona meseji ya Chinga kwenye simu yangu
iliyosema. “Usiwe mkali jifanye mjinga kwa akili yako. Nimeshakuambia
nitakuhamishia Masaki”
Kwa sababu maji yalikuwa shingoni na sikuwa na la kufanya, yale
maelezo ya Chinga yalinifariji kidogo ingawa nilijua Chinga hakuwa mtu wa
kuaminika.
Nilitoka ukumbini ili niende msalani.Nikashituka nilipomuona
Chinga amevaa taulo na Vicky aliyevaa khanga moja tu wakitoka chumbani na
kuelekea sebuleni huku wakizungumza na kucheka.
Wamerudi saa ngapi? Nikajiuliza kwa mshangao.
Nikahisi bila shaka Chinga alirudi usiku wakati nikiwa
nimelala.Akampitia mke wake huko kwa dada yake alikokwenda kisha wakaja
pamoja.Kwa vile funguo alikuwa nayo, Chinga hakuwa na haja ya kunigongea
mlango.Waliweza kufungua mlango na kuingia ndani bila mimi kujua.
Kile kitendo cha kuwakuta wamelala pamoja kilinichoma roho, nikajiona
kama nimeshatemwa isipokuwa ninadanganywa tu.
Lakini nikajiambia nifuate vile Chinga alivyoniambia kuwa
nijifanye mjinga kwa akili yangu ili nione mwisho utakuwa nini.Nikaenda
msalani. Nilipotoka nikaanza kufanya usafi. Nilipofika sebuleni niliwasalimia
kisha nikaendelea na usafi.
Nilipomaliza kazi hiyo Chinga alinituma vitafunio nikaenda
kununua. Niliporudi niliandaa chai mezani. Chinga akaniambia tunywe pamoja,
tukaenda kunywa na mke wake.Wenyewe walikuwa wanazungumza mimi nilikuwa kimywa.
Baada ya kunywa chai niliondoa vyombo nikaenda kuviosha.
Nilipomaliza Chinga alinipa pesa niende sokoni. Niliporudi sokoni niliingia
jikoni. Chinga na Vicky wakatoka. Sijui walikwenda wapi.Walirudi saa saba
mchana wakati nilikuwa nimeshamaliza kupika
Nikataka kwenda kuwaandalia chakula lakini Chinga akaniambia
wameshakula huko walikotoka na kwamba chakula nilichopika tutakula jioni.
Nikashukuru kwani kazi ya utumishi sikuipenda, nikaenda kula peka
yangu.
Tulishinda salama hadi usiku. Baada ya kumaliza kula chakula cha
usiku, rafiki zake Chinga walitokea.Chinga akamueleza mke wake kwamba wenzake
wamemfuata kwa ajili ya safari ya kwenda Kibaha ambako walikuwa na shughuli
zao.
“Utarudi saa ngapi?” Vicky akamuuliza.
“Kwenye saa saba au nane hivi”
“Sawa”
Chinga na rafiki zake wakatoka.
Ilipofika saa tano usiku mimi na Vicky tuliingia vyumbani kulala. Kama kawaida yangu nilikaa kitandani kwa muda mrefu bila
kupata usingizi kutokana na kusongwa na mawazo.
Wakati usingizi unaninyemelea nilisikia mlango wa mbele unagongwa
kwa kishindo. Nikatega masikio na kusikiliza. Mlango ukaendelea
kugongwa.Nikainuka na kukaa kitandani.Niliposikia Vicky anafungua mlango wa
chumbani mwao na mimi nilifungua mlango.
“Ni nani?” nikamuuliza.
“Ni John amenipigia simu, anasema amepigwa risasi ya bega” Vicky
akanijibu.
Tukiwa tumeshituka tukaenda kufungua mlango.Tulimkuta John
ameanguka chini kando ya mlango baada ya kuishiwa na nguvu. Mkono wake wa kulia
alikuwa ameshika simu wakati bega lake la mkono wa kushoto lilikuwa linavuja
damu ambayo iliunda mchirizi kuanzia alikotokea.
“Niingizeni ndani haraka!” akatuambia.
Wakati tunamshika ili tumuingize ndani tukasikia mbwa anabweka.
Kutupa macho tuliona polisi wanne mmoja amemshikila mbwa aliyekuwa akiwaongoza
kufuatilia ile njia aliyokuwa ameipita Chinga. Nyuma ya polisi hao kulikuwa na
gari ya polisi inayowafuata.
Kutokana na mwanga wa taa iliyokuwa inawaka mbele ya nyumba yetu, polisi
hao walituona. Nikamuona Chinga akiachia simu na kutia mkono ndani ya shati lake akatoa
bastola aliyompa mke wake.
“Ficha hii bastola!” akamwaambia.
Vile Vicky anaipokea tu bastola hiyo, sauti ya mmoja wa polisi hao
ikatuamuru.
“Nyote mikono juu, mko chini ya ulinzi!”
Polisi hao walikuwa wameshafika karibu na mbwa aliyekuwa
akimbwekea Chinga aliyekuwa amelala chini. Polisi wawili miongoni mwao walikuwa
wametuelekezea bunduki.
Vicky alibaki na bastola aliyopewa na Chinga akiwa hajui la
kufanya. Mimi niliinua mikono juu huku nikitetemeka. Sikujua nini kilikuwa
kimetokea.
“Nyinyi wanawake ndiyo mnaofuga majambazi!” mmoja wa polisi hao
akatuambia.
“Nani jambazi!” nilithubutu kumuuliza.
Hapo ndipo tulipoelezwa na polisi hao kwamba Chinga alikuwa
jambazi na kwamba yeye na wenzake watatu walikwenda kuvunja duka moja pale
Sinza lakini tayari walikuwa wamewekewa mtego na polisi. Wakavamiwa na kuanza
kutupiana risasi na polisi. Chinga akapigwa risasi ya bega na kukimbia. Wenzake
wawili waliuawa na mmoja alikimbia na gari walilokuwa nalo.
Lo! Sikujua,kumbe Chinga ni jambazi? Nikawaza.
Ni kwa sababu tu ya tamaa yangu ya kupenda pesa sasa nimejiingiza
katika matatizo yasiyonihusu na nisiyo yajua.
Wakati tunamshika ili tumuingize ndani tukasikia mbwa anabweka.
Kutupa macho tuliona polisi wanne mmoja amemshikila mbwa aliyekuwa akiwaongoza
kufuatilia ile njia aliyokuwa ameipita Chinga.Nyuma ya polisi hao kulikuwa na
gari ya polisi inayowafuata.
Kutokana na mwanga wa taa iliyokuwa inawaka mbele ya nyumba
yetu,polisi hao walituona. Nikamuona Chinga akiachia simu na kutia mkono ndani
ya shati lake akatoa bastola aliyompa mke wake.
“Ficha hii bastola!” akamwaambia.
Polisi hao walikuwa wameshafika karibu na mbwa aliyekuwa
akimbwekea Chinga aliyekuwa amelala chini.Polisi wawili miongoni mwao walikuwa
wametuelekezea bunduki.
Vicky alibaki na bastola aliyopewa na Chinga akiwa hajui la
kufanya. Mimi niliinua mikono juu huku nikitetemeka. Sikujua nini nilikuwa
kimetokea.
“Nyinyi wanawake ndiyo mnaofuga majambazi!” mmoja wa polisi hao
akatuambia.
“Nani jambazi!” nilithubutu kumuuliza.
Hapo ndipo tulipoelezwa na polisi hao kwamba Chinga alikuwa
jambazi na kwamba yeye na wenzake watatu walikwenda kuvunja duka moja pale
Sinza lakini tayari walikuwa wamewekewa mtego na polisi. Wakavamiwa na kuanza
kutupiana risasi na polisi. Chinga akapigwa risasi ya bega na kukimbia.Wenzake
wawili waliuawa na mmoja alikimbia na gari walilokuwa nalo.
Lo! Sikujua,kumbe Chinga ni jambazi? Nikawaza.
Ni kwa sababu tu ya tamaa yangu ya kupenda pesa sasa nimejiingiza
katika matatizo yasiyonihusu na nisiyo yajua.
Baada ya polisi kutupa maelezo yaliyoonyesha kuwa Chinga
alikuwa ni jambazi na alipigwa risasi wakati yeye na wenzazke
walipojaribu kuwashambulia polisi, Chinga alibebwa juu juu
na kupakiwa ndani ya gari ya polisi.
Vicky aliyekutwa na ille bastola mkononi aliulizwa alikuwa
akihusianaje na Chinga, akajibu kuwa alikuwa mume wake.Yeye naye akakamatwa..Mimi
nilipoulizwa nilieleza kuwa nilikuwa mtumishi wa ndani. Jibu hilo ndilo lililonisalimisha nikaachwa nibaki
na nyumba.Lakini nilitakiwa kufika kituo cha polisi cha Sinza saa mbili asubuhi
na nimuulizie Inspekta Amour.
ITAENDELEA
No comments:
Post a Comment