Saturday, November 12, 2016

DONALD TRUMP WA AINA, HATAKI DOLA HATA MOJA , AUKACHA MSHAHARA WA URAIS

Sihitaji hata dola moja kwenye mshahara wangu nikiingia Ikulu” Donald Trump

“Sitachukua hata Dola moja kwenye mshahara wa Urais”, ni kauli ya Rais mteule Donald Trump baada ya kuulizwa kwamba atakuwa akiufanyia nini mshahara wa Dola laki nne (400,000 kwa mwaka) ambazo ni mshahara wa Rais wa Marekani anapokuwa Ikulu ya White House.
Kauli hii aliitoa Donald Trump mshindi wa kiti cha Urais nchini Marekani wakati akiwa kwenye kampeni zake September 17, 2015, huko Rochester, New Hampshire: “Kitu cha kwanza ninachotaka kuwaambia na nitakifanya kama nikichaguliwa kuwa Rais, Sitakuwa nikichukua mshahara, hata dola moja siihitaji, hicho sio kitu kikubwa kwangu.” – Donald Trump

No comments:

Post a Comment