Tangakumekuchablog
Dar es
Salaam, MKURUGENZI wa habari na Maelezo, Hassan Abass, amewataka waendeshaji wa
mitandao ya kijamii (bloggers) kuheshimu misingi ya taaluma ya upashaji habari.
Akizungumza
katika kongamano kwa wanachama wa mitandao ya kijamii (TBN), Abbass ameitaka
mitandao hiyo kuhakikisha habari zao zinasaidia jamii katika nyanja mbalimbali
za afya , elimu na mazingira.
Alisema
mitandao ya kijamii iko na umuhimu mkubwa kwa jamii hivyo kuwataka kuhakikisha
habari zao zinakuwa za ukweli na weledi jambo ambalo litaweza kuisaidia jamii.
“Nimefurahi
kukutana na waendeshaji mitandao ya kijamii natambua kuwa muko na mchango
mkubwa kwa jamii na Serikali hivyo fanyeni kazi zenu kwa weledi” alisema Abass
Alisema ili
kufanya kazi kwa weledi ni vyema kuongeza elimu lengo likiwa ni kufanya kazi
kwa umakini na umahiri na kuleta changamoto za upashanaji wa habari.
Awali
akizungumza katika mkutano huo, mwenyekiti wa Mtandao wa kijamii (TBN) , Joaqim
Mushi, alisema mitandao ya kijamii imekuwa katika nafasi kubwa ya upatikanaji
wa habari kwa wakati.
Alisema mitandao
ya kijamii imekuwa na changamoto nyingi za upatikanaji wa habari hivyo kutaka
kila Mkoa kwenye shughuli za kitaifa kupewa nafasi.
“Kupitia kongamano hili naiomba Serikali
kuitambua mitandao ya kijamii na kupewa nafasi katika shughuli za kitaifa, hii
itasaidia jamii kupata habari” alisema Mushi
Mushi
aliwataka waendeshaji mitandao ya kijamii kujikita katika habari za vijijini
ambako kuna changamoto nyingi zikiwemo za kilimo na ukosefu wa huduma za
kijamii ikiwemo maji.
Mwisho
No comments:
Post a Comment