Saturday, December 3, 2016

WAANDISHI WA HABARI TANGA WAASWA

 Tangakumekuchablog

Tanga, MWENYEKITI wa Klabu ya Waandishi wa Habari Tanga (TPC), Hassan Hashim, amewatakla waandishi wa habari wa Tanga kupendana na kuacha kufanyia majungu.
Akifungua mkutano mkuu wa wanachama wa Tanga Press Club (TPC) jana, Hashim alisema tabia ya baadhi ya waandishi kutiliana majungu haipendezi na kuondosha sura nzima ya fani ya uandishi wa habari.
Aliwataka kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwao ili kuweza kuyafikia malengo yao pamoja na kuutangaza Mkoa wao katika nyanja mbalimbali za kiuchmi na maendeleo.
“Ni jambo la kuhuzunisha na aibu kwa waandishi kutiliana majungu, nah ii haijengi bali inabomoa hivyo kwa pamoja tubadilike kwani sisi ni kioo cha jamii” alisema Hashim  na kuongeza
“Jambo la kufurahisha ni kuona klabu yetu imesimama vizuri na kuna hatua kubwa ya kimaendeleo imefikiwa hivyo niwatake wanachama na wasio wanachama kushikamana” alisema
Akizungumzia kuhusu changamoto na kero za waandishi , mwenyekiti huyo aliwataka wajumbe hao wa mkutano kuyazungumza mambo yao katika vikao halali vya klabu na kuacha kusema pembeni.
Alisema kunung’unika  pembeni hakujengi bali hubomoa na kuwapa faida watu pembeni  hivyo kuwataka kutambua kuwa hakutakuwa na mtu pembeni atakaetatua matatizo yao zaidi ya klabu yao.
Katika mkutano huo wajumbe walishauri kutoa adhabu kali kwa mwandishi atakaekiuka maadili ya fani ya uandishi ikiwemo kupandikiza migogoro ndani ya klabu na nje ya klabu.
                                       Mwisho



  Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari  wa Tanga Press Club , Hassan Hashim, akifungua mkutano mkuu wa wanachama wa (TPC) mktano uliofanyika ukumbi wa klabu hiyo. Kushoto ni Katibu wa TangaP Prees Club, Anna Makange na Mweka Hazina , Zawadi Kika

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Tanga, Hassan Hashim (kushoto) , akiwaongoza wanachama wa Tanga Press Club (TPC) sala kumuombea mwanachama mwenzao, Pitter Mohamme aliefarikimwishoni mwa mwezi uliopita wakati wa mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika


No comments:

Post a Comment