Friday, July 17, 2015

UBAGUZI MAREKANI SASA UMEFIKIA KIKOMO

Meya wa Washington kamuita Obama nyani, ataachwa?

Barack-Obama
Rais Barrack Obama
Patrick Rushing ni Meya wa Mji wa Airway Heights ambao uko Washington, jamaa alijikuta tu akimwita Obama nyani na akamwita Michelle Obama sokwe !!
Ukizungumzia ishu ya Ubaguzi wa rangi Marekani sio kesi ndogo, lakini Meya Rushing amesema yeye sio mbaguzi japo aliyaandika haya kwenye ukurasa wake Facebook >>>> “Huyu mwanamke Michelle mwenye uso wa sokwe hamvutii mtu yoyote labda Obama mwenye uso wa nyani.. waangalie masikio yao, LOL” >Patrick Rushing.
Ikainuka stori ya Halmashauri ya Jiji kumtaka ajiuzulu >>>> “Nakubali kwamba nimekosea, ila kama nikijiuzulu itaonekana kama mimi ni mbaguzi wakati sio kweli… Huo ni utani ambao huwa tunafanya na rafiki zangu kila mara” >>>> Meya Rushing.
patrick-rushing
Patrick Rushing
Gazeti moja la Marekani lilitembelea ukurasa wake wa Facebook na kukuta post zaidi ya 75 zikihusiana na ubaguzi wa rangi, Wahamiaji wanaoishi Marekani, zipo alizomponda Hillary Clinton na pia nyingine kawaponda wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.obama-basketball_2773422b
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment