Daraja la Amboni mto
Mkurumuzi barabara ya Tanga - Horohoro
kingo zake zikiwa zimebomoka baada ya kugongwa na gari ambayo ilifeli
breki wakati ikishusha mlima.
Daraja hilo ambalo liko njia ielekeayo Mombasa Kenya mji wa kibiashara na moja ya Msoko ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa muda mrefu limekuwa katika kitisho kwa watumiaji wa vyombo vya moto.
Chini ya Daraja hilo ambalo kuna mto Mkurumuzi inasemekana kuna mamba hivyo kuongeza kitisho cha hatari itokeapo ajali.
Mkazi wa Amboni Tanga, Ramadhani Issa, akiangalia kingo za daraja la Amboni mto Mkurumuzi barabara ya Tanga- Horohoro ambazo zimebomoka kwa kugongwa na gari baada ya kufeli breki wakati ikishusha mlima.
No comments:
Post a Comment