Maswali na majibu yote ya Rais Magufuli aliyowajibu Waandishi wa Habari leo Ikulu, Dar
Rais Magufuli: Niwashukuru sana kwa michango yenu mikubwa katika maeneo yenu ya kazi.
Swali(Tido Mhando): Ulichukua muda kuunda baraza la mawaziri, Je Katika tathmini hiyo wanafanya kazi kulingana na ulichotegemea wakifanye
Jibu(Magufuli): Serikali niliyounda imenisaidia sana na wanafanya
kazi zao vizuri, niliona niwe na baraza la watu wachache katika
kuwatumikia wananchi, changamoto zipo lakini nina imani kubwa.
Swali(Lulu Sanga TV 1): Kuna changamoto kubwa sana ya dawa,
watoto wengi wanakufa kutokana na kukosa dawa, unaoneje ukibana matumizi
kupata dawa ukazigawa hospitali kubwa au kampeni kama ile ya madawati.
Jibu(Rais Magufuli): Katika bajeti yetu tumetenga bilioni 1.99 na
tumeongeza bajeti ya kununulia madawa karibu mara kumi. Tumebadilisha
utaratibu badala ya kununua kutoka kwa suppliers sasa tunanunua moja kwa
moja kutoka viwandani pia kuna nchi zinataka kuwekeza kujenga viwanda
vya kutengeneza madawa hapahapa.
Swali kuhusu kukandamiza demokrasia:
Jibu: Katika kazi yoyote Sijakandamiza demokrasia ndio maana
unaona bunge linaendelea na chaguzi zinaendelea hata hapa wamechagua
UKAWA, demokrasia ina mipaka yake, baada ya uchaguzi lazima watu
waendelee na production
Swali(Tido)-Nyongeza: Kuna watu wanasema unataka kuelekea kwenye udikteta
JIBU: Tafsiri kila mmoja ana yake na kila mmoja ana uhuru wa
kufukiria anavyofikiria hata wewe Tido ulihama BBC, TBC na sasa uko
Azam, mwingine anaweza kufikiri uko ulikokuwa kulikuwa na udikteta wa
aina fulani.
Swali(Rioba): Unasisitiza uchumi wa viwanda, Tanzania imeshawahi
kuwa na viwanda vikafa, kuna watu wanaona hili swala waachiwe watu
binafsi, wewe unaoneje?
Jibu: Ilani inasema tunataka kujenga nchi ya viwanda, huwezi
kutegemea serikali katika kujenga viwanda ndio maana nikasema kuna
makampuni kutoka Kenya na sio makampuni ya watu binafsi.
Swali(Mtanzania): Serikali imeweka mkazo kwenye kupambana na majangili lakini tishio ni kubwa,
Jibu(Rais Magufuli): Umezungumza ukweli na ni changamoto ila pia ina
historia yake, sheria ya mifugo ya mwaka 59 ila tumejipanga kuhakikisha
haya masuala yasije yakawa parmanent na tumeibadilisha wizara ya
maliasili na nimeteua majenerali kuongoza wizara nadhani umeshajua
tunataka kufanya nini. Hatuna viwanda vya nyama nchi hii ndio maana
mifugo haina pakwenda.
Swali(Magazeti ya serikali): Ni nini mkakati wa kuwafanya watanzania kuona fursa katika sekta nyingine
Jibu(Rais Magufuli): Sisi kama serikali ni kuwaelimisha waweze
kutumia fursa zilizopo katika nchi nyingine, mfano sisi tunasifika
kwenye Kiswahili, kila mmoja ajipange badala ya kusubiri serikali. Fursa
zipo ikiwemo EAC na SADC ambako Tanzania ni mwanachama. Ni wajibu sisi
wa watanzania kuchangamkia fursa.
Swali(Tido Mhando): Ulitilia mkazo Rushwa na ufisadi, mwaka mmoja sasa unasemaje?
Jibu(Rais Magufuli): Matunda yameanza kuonekana, nidhamu kazini
imeanza kuonekana, tumepitisha sheria ya mafisadi na kesi ya kwanza
imeanza kusikilizwa jana. Rushwa na swala mtambuka na haliwezi
kushughulikiwa na Rais peke yake. Nitoe wito kwa watanzania wote tukatae
Rushwa, ni kansa ya maendeleo.
Swali(Rioba): Kuna maswala umeyasimamia kwa ujasiri ikiwemo ujangili na dawa za kulevya, nini kinakuumiza kichwa
Jibu(Rais Magufuli): Yanayoniumizwa kichwa ni mengi pamoja na
swali lako, yale niyoahidi katika miaka mitano bado sijayamaliza na
hayawezi kumalizika ndani ya mwaka mmoja. Kwenda mbele unahitaji support
ya watu wengi. Mwenyezi Mungu pamoja na support ya watanzania.
Swali(Tuma-Radio Tumaini): Hongera sana, Kura yangu ilifanya
kazi, Walemavu wa chini hali bado ni mbaya, tunazo sheria nyingi
tunaishukuru serikali. Mazingira yetu(walemavu) bado ni magumu, tunaomba
watu wa chini watu iwaangalie.
Jibu(Rais Magufuli): Nimelipokea ombi lako na tutaendelea
kulishughulikia na serikali inajali sana walemavu kwani hata sisi ni
walemavu wa kesho, nimeunda wizara maalum ya walemuavu, nimewateua
walemavu katika baraza langu ikiwemo Dr Possy, Amon Mpanju.
Swali(Bakari Machumu Mwananchi): Viwanda na utajiri wa madini,
umeelezea umuhimu wa PPP, kuna wafanyabiashara wanahisi wanatengwa,
upande wa madini, tunaunganisha vipi
Jibu(Rais Magufuli): Wafanyabiashara hawajatengwa na tunawahitaji
sana, na mimi nawapenda kweli wafanyabiashara lakini nataka wanaolipa
kodi. Mfanyabiashara ambae hajalipa kodi anawaumiza ambao wamelipa kodi,
ukishakua na wafabiashara wa aina mbili unawaumiza wanaolipa. Palikuwa
na mamabo ya hovyo, sitaki kwenda kwenye detail sana maana mambo mengine
yapo mahakamani, wafabiashara matapeli siwapendi.
Jibu(Rais Magufuli): Kuhusu madini, ni kweli nchi hii ina madini
mengi sana, madini yanatakiwa kunufaisha nchi hii, siku moja yatakwisha,
nina uhakika sasa mambo yataanza kwenda vizuri baada ya kusaini
regulations. Sisi tuna mafuta pia, tutaunganisha bomba la hoima kwenda
Tanga, Tanzanite inapatikana Tanzania tu lakini nchi iliyoongoza kuuza
ni India ikifuatiwa na Kenya.
Sasa hivi umeanzishwa mnada hapa. Watu wanasafirisha makontena kwenda
nje kusafishwa na sisi wenyewe tunayasindikiza. Kwa nini tusitengeneze
hapa, haya ndio ndio najaribu kuyazungumza ili nchi yetu isiendelee
kuibiwa, kwenini kila sehemu kwenye madini kuna kiwanja cha ndege, hili
sio suala la Rais pekee ili pesa zinazopatikana ziwanufaishe watanzania
wote. Unachosema ni sawa na kinachotakiwa sasa kusonga mbele.
Swali(Joseph Kulambwa): Tanzania ya viwanda, serikali imejipangaje kutrain mafundi mchundo kuliko wasimamizi wa viawanda
Jibu(Rais Magufuli): Vyuo vya kati tulivibadilisha kuwa vyuo
vikuu, ilikua bad direction ndio maana sasa tunajenga vyuo vya VETA
ikiwezekata kila mkoa. Hata chuo cha usafirishaji kimekua chuo kikuu na
inawezakana kwa sababu kulikua na mikopo ambayo hairudishwi ndio maana
sasa kuna deni la trilioni 3.5.
Swali: Wafanyakazi hewa wameondolewa lakini bado mishahara inayolipwa ni mikubwa?
Jibu(Rais Magufuli): Siku za nyuma kuna madai mengi ambayo
yamepelekea serikali kulipa kiasi cha bilion 22.6 na bado kuna madai
39,000 yenye thamani ya sh bilioni 23
Suala la OC bado halitakuwepo kwani mambo yanaenda vizuri.
Aidha serikali itaendele kulipa madeni ya walimu na wakandarasi wanaodai.
Swali(Angalieni Mpendu): Suala la utamaduni na maadili, umeliwekaji katika utawala wako?
Jibu(Rais Magufuli): Jukumu la ku-maintain utamaduni wetu ni la
kila mtanzania, kuna wizara inayoshughulika suala hili. Kila mtanzania
ana wajibu wa kutunza utamaduni wetu.
Vyombo vya habari vitoe ushrikiano kwa kuhakikisha utamaduni wetu unakuwa mzuri.
Swali(Bukuku): Serikali ya china na Tanzania ni Marafiki,
Unaonaje kama ungefanya mazungumzo ma Wachina kukawa na ushirikiano
katika mafunzo na mashine ndogondogo?
Jibu(Rais Magufuli): Nimeshazungumza nao, wachina wamekubali na
wanataka kuchukua eneo la Bagamoyo wajenge viwanda 1000. Pia
tumezungumza na serikali ya India katika suala kama hilo hilo.
Tumezungumza na serikali ya Morocco na kutakuwa na ndege ya moja kwa
moja kutoka Kasablanca hadi JNIA.
Tumeweka fedha katika benki ya TIB kwa ajili ya kukopesha wajasiriamali.
Tatizo ni kwamba watu wanakopa lakini hawarudishi ikiwemo wanasiasa.
Tatizo la waandishi wa habari hawaaniki watu hawa.
Swali(Tido Muhando): Mchakato wa katiba Mpya umefikia wapi?
Jibu(Rais Magufuli): Katika kampeni yangu hakuna sehemu ambayo
nimezungumzia suala la Katiba Mpya, hata hivyo suala la katiba mpya
limefika mahali pazuri lakini niacheni kwanza ninyooshe nchi.
Swali(Edoni Mwanika): Kwa nini miswada ya habari inakuwa haipewi muda wa kutosha kujadiliwa na huletwa kidharura tu?
Jibu(Rais Magufuli): Sheria yeyote ina misingi yake, mchakato wa
sheria hizi umeanza toka mwaka 2010 hadi mwaka huu, hakuna muda sahihi
ungetosha kujiandaa.
Hata hivyo hili ni suala ambalo lipo ndani ya maamuzi ya bunge hivyo siwezi kuingilia,
Punde musuada huu utakaponifikia nitaisaini na kama ni marekebisho yatafuata.
Swali(Frank): Umeokoa kiasi gani kwa kutosafiri nje? umechukua
hatua gani kuhakikisha ukanda wa Afrika mashariki unakuwa salama? Suala
la diaspora kutoweza kuwa tena raia wa Tanzania unalizungumziaje?
Jibu(Rais Magufuli): Fedha tulizookoa ni mabilioni, hata hivyo
siyo kwamba hatusafiri kabisa ila tunahakikisha kunakuwa na uwakilishi
ambao unapunguza gharama.
Tumekuwa tunashughulikia migogoro inayoendelea, DRC nimemtuma mwenyekiti
wa mawaziri kwenda ili kutafuta suluhu. Suala la migogoro linadiliwa
mezani, Burundi tumemteua Mh Mkapa na anasuluhisha na mambo yanaenda
vizuri.
Kuhusu diaspora lipo kisheria zaidi.
Swali(Sanga): Una maoni gani katika ishu ya Zanzibar na Utawala bora?
Jibu(Rais Magufuli): Hali ya Zanzibar ni nzuri, wamefanya uchaguzi wao vizuri na Dr Shein anafanya vizuri na mambo yanaenda vizuri
Swali(Manyere): Upi ni msimamo wetu kuhusu Morocco; Je Ikulu haiwezi kuandaa tuzo kwa waandishi wanaondika mambo mazuri kuhusu nchi?
Jibu(Rais Magufuli): Tanzania ni nchi isiyofungamana na upande wowote na hivyo tuna uhuru wa kushirikiana na nchi yeyote.
Hata hivyo Moroco tunashirikiana nao katika kukuza biashara
Vyombo vya habari vinafanya kazi nzuri kwelikweli,
Nashirikiana na kila mtu hata Masoud anavyonichora kichwa kimevimba hapa, nashirikiana naye.
Swali(Pasco Mayala): Ulitumia mamlaka gani kuamuru bunge na mahakama kufanya unayoyataka? ulitumia mamlaka gani kuzuia mikuatana ya kisiasa?
Jibu(Rais Magufuli): Serikali ndiyo inahusika na kugawa fedha zote kupitia bajeti, fedha zikitumika vibaya anayehusika ni serikali.
Swali: Unalizungumziaje suala la ajira? Umekuta mambo yapoje ikulu? Na ulikuwa unatazamia nini
Jibu(Rais Magufuli): Ajira zilikuwa hazijazuiliwa, serikali imetoa ajira za madaktari na manesi wa hospitali ya Rweganzira.
Zuio la ajira lilikuwa la muda tuu. Mpaka sasa kuna benki iliyorudisha fedha za wafanyakazi hewa kiasi cha shilingi bilioni 6.7.
Serikali inaajiri kwa uangalifu mkubwa ili kuhakikisha suala la wafanyakazi hewa
Serikali imeajiri zaidi za watumishi 5000 kwenye vyombo mbalimbali.
Serikali inaendelea kuboresha maslahi ya wakulima kwa mfano wa korosho;
Kilo ya korosho imeongezeka bei kutoka shilingi 600 hadi sh 4000.
source mgblog
No comments:
Post a Comment