Msajili wa vyama vya siasa amefuta usajili wa vyama vitatu
Leo November 9 2016 Msajili wa
vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi ametangaza kuvifutia
usajili wa kudumu vyama vya Chama cha haki na ustawi ‘CHAUSTA’, African
Progressive Party of Tanzania ‘APPT Maendeleo’ na Chama cha Jahazi
Asilia.
Taarifa aliyoitoa Jaji Mutungi imesema
kwamba Mchakato wa kufuta usajili wa kudumu wa vyama hivyo unatokana na
zoezi la uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa
mengine ya kisheria ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu
uliofanyika kuanzia June 26 mpaka July 26 2016.
Jaji Mutungi ameeleza kuwa zoezi hilo la
uhakiki ilibainika kuwa, vyama vya siasa hivyo vitatu vimepoteza sifa
za usajili wa kudumu kwa kukiuka masharti ya sheria ya vyama vya siasa,
hivyo kila chama kilipewa taarifa ya nia ya msajili kufuta usajili wake
wa kudumu na kutakiwa kujieleza kwa nini kisifutiwe.
Taarifa ya Jaji Mutungi imesema katika
utetezi wao vyama hivyo vilishindwa kutoa sababu za kuridhisha kuwa
havijakiuka sheria na bado vinazo sifa za usajili wa kudumu.
millardayo
No comments:
Post a Comment