Chama cha Republican kudhibiti tena congress Marekani
Chama cha Republican kimenyakua tena uwingi wa viti katika Bunge la Wawakilishi la Marekani, kulingana na makadirio.
Vituo vya televisheni za Marekani ABC na NBC kwa pamoja zimekadiria kuwa Republican itakuwa na viti 435-katika bunge hilo, idadi ambayo chama hicho kimekuwa nayo tangu mwaka 2010.
Republican pia wanaendelea kushikilia udhibiti wake wa Bunge la Seneti, licha ya kwamba Democrat wanatumai kufaulu.
Kwa kuwa Donald Trump amepata ushindi wa urais ataongoza nchi kwa urahisi kutokana na kwamba sasa bunge lote la Congress liko mikononi mwa Republican.
Usiku wa uchaguzi ulianza kwa ushindi huo huku Republican wakinyakua viti 34 kati ya 100.
Hata hivyo kadri kura zilivyoendelea kutangazwa Tammy Duckworth mgombea wa Democrat, mpiganaji wa zamani wa vita vya Iraq ambaye alipoteza miguu yake yote miwili, alichukua nafasi ya Mark Kirk wa Republican katika jimbo la Illinois.
Wakati wa mdahalo wa televisheni mwezi uliopita Bwana Kirk alimkejeli Duckworth kwa kuwa na asili ya Thailand , lakini baadae aliomba msamaha.
Spika wa Bunge la Congress Paul Ryan, ambaye alijitenga na bwana Trump wakati wa kampeni baada ya kumidhinisha awali , amechaguliwa tena katika uchaguzi wa Bunge la Wawakilishi katika jimbo la Wisconsin.
Ilhan Omar amekuwa mwanamke wa kwanza mmarekani mwenye asili ya kisomali kuchaguliwa kama mbunge, kwa kupata ushindi katiika jimbo la Minnesota.
Alifika Marekani wakati alipokuwa bado mtoto, alipotoroka vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Somalia akiwa pamoja na familia yake na kuishi miaka minne katika kambi ya wakimbizi nchini Kenya.
Udhibiti wa Congress unaangaliwa kama suala nyeti kwa mipango ijayo ya rais hususan kufanya mabadiliko ya sera kuwa sheria.
No comments:
Post a Comment