Nilvado ambaye hakusafiri na wachezaji waliofia katika ndege, ametangaza kustaafu
Golikipa wa mkongwe wa klabu ya Chapecoense ya Brazil Nilvado ambaye hakuwa amesafiri na timu kuelekea Colombia na wenzake kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza wa klabu Bingwa America Kusini Sudamericana ametangaza kustaafu kucheza soka.
Nilvado mwenye umri wa miaka 42 alijiunga na Chapecoense
mwaka 2006 na alikuwa ameichezea timu hiyo jumla 299 na alikuwa
anasubiri acheze mechi moja ya mwisho ili atimize jumla ya mechi 300
akiwa na aagwe na kustaafu soka.
Kipa huyo hakucheza mchezo wa Jumapili wa ugenini dhidi ya Palmeiras uliomalizika kwa timu yake ya Chapecoense kupoteza kwa goli 1-0 ili acheze mchezo wake wa 300 na kuagwa rasmi akiwa katika uwanja wao wa nyumbani mbele ya mashabiki wao.
No comments:
Post a Comment