Tangakumekuchblog
Tanga, KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya
Wanawake, Fair Play Queens ya Tanga inayoshiriki ligi ya Wanawake Tanzania
Bara, Kuha Idd, amesema siri ya kuibugiza mabao manne Mburahati Queens ni
mazoezi kutwa mara tatu.
Akizungumza
mara baada ya kipenga cha mwisho wa mchezo, Idd alisema ushindi huo mnono
haukuwa rahisi bali ni juhudi za wachezaji wake kuhimili dakika 90 bila
kuchoka.
Alisema mara
nyingi amekuwa akiwaeleza wachezaji wake kuwa siri ya ushindi uwanjani ni kuwa
na pumzi na kucheza kwa ari hata kama umetanguliwa kufungwa.
“Mburahati
waliuanza mpira kwa kasi na mimi nilijua kwani wamekuwa wakipoteza mechi
mfululizo na leo walitaka kuondoa jinamizi kwetu lakini nasi tulijipanga”
alisema Idd
Aliwataka
washabiki wa timu hiyo kuwapa moyo wachezaji wake kwa kujitokeza kwa wingi kila
wanapocheza ili kujiweka vizuri katika mashindano hayo.
Katika hali ya
kushangaza, Kocha wa Mburahati Queens, Nokha Kanyaga, amekataa kuzungumza na
waandishi wa habari na kusema kuwa hana cha kusema kwani kila mmoja mpira
aliuona kwa macho yake.
Timu hiyo
imefungwa mabao 4 kwa 2 na kulalamika unapofungwa mabao mengi kama mvua huna
cha kuzungumza na kubaki kumshukuru Mungu.
“Niseme nini
na kila mmoja ameona kwa macho yake kwani palikuwa na kipofu hapa, nasema sina
cha kuzungumza na tuacheni nawambia” alisema Kanyaga
Alisema
mpira umeisha na tumefungwa lakini hawezi kuzungumzia dakika 90 za uwanjani na
kudai kuwa kila mmoja atakuwa hakimu wa mchezo.
Mwisho
Kiungo
wa timu ya Fair Play ya Tanga, Mwanaisha Mussa, akiwachomoka wachezaji wa
Mburahati Queens wakati wa mchezo ligi ya wanawake uwanja wa Mkwakwani juzi,
Fair Play aliibuka na ushindi wa mabao 4
, 2.
Mshambuliaji wa Mburahati Queens, Mwantumu Seng’enge akimtoka mchezaji wa Fair Play, Mwanaisha Mussa wakati wa mchezo ligi ya Wanawake uwanja wa Mkwakwani juzi, Fair Play ilishinda mabao 4, 2.
Mshambuliaji wa Mburahati Queens, Mwantumu Seng’enge akimtoka mchezaji wa Fair Play, Mwanaisha Mussa wakati wa mchezo ligi ya Wanawake uwanja wa Mkwakwani juzi, Fair Play ilishinda mabao 4, 2.
Kikosi cha Mburahati Queens
No comments:
Post a Comment