Mwanafunzi alitaka Selfie ya kipekee juu ya Mlima…kilichofuata ni Story!!
Matumizi ya picha za Selfie sasa yameanza kuleta madhara kwa baadhi ya watu ambao hutamani kupiga picha za kipekee za aina hiyo.
Pamoja na upigaji wa picha hizo kuzidi
kuongeza umaarufu katika maeneo mengi duniani lakini kuna stori nyingi
ambazo zimekua zikitokea zinazohusu watu kupoteza maisha kutokana na
jinsi wanavyopiga picha hizo.
Tangakumekuchablog iliwahi
kuandika stori ya binti mmoja kupoteza maisha baada ya kutamani kupiga
picha ya selfie ya kipekee ambapo alipanda juu ya treni iliyokua
ikitembea ili tu aweze kupata picha hiyo na badala yake alipoteza maisha
baada ya kupigwa na shoti ya umeme huku wenzake wakijeruhiwa vibaya.
Leo tena kumetoka Stori inayofanana na
hiyo baada ya mwanafunzi mmoja wa chuo huko Indonesia kupoteza maisha
baada ya kujaribu kupiga picha ya selfie kwenye ukingo wa mlima ambao
kwa chini kulikuwa na bahari.
Mohamed Aslam ambaye ni
raia wa Singapore alifikwa na mauti baada ya kudondoka baharini ikiwa
ni urefu wa futi sita wakati akichukua picha hiyo katika visiwa vya Lembongan.
Baadhi ya mashuhuda ambao walikua
marafiki zake walisema mwanafunzi huyo alikufa baada ya kutokea upepo
mkali uliomdondosha na baadaye mwili wake ulipatikana pembezoni mwa
bahari hiyo na alipofikishwa hospitali tayari alikua amefariki.
Kwa habari na matukio kedekede ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment