Monday, May 25, 2015

KIPIGO CHAMFUKUZISHA BRENDAN RODGERS

Brendan Rodgers kuihama Liverpool?

roger
Kipigo cha aibu walichokipata Liverpool dhidi Stoke City jana kimepelekea kocha wao Brendan Rodgers kutamka maneno mazito juu ya hatma yake ndani ya klabu hiyo.
Kocha huyo amesema yupo tayari kuondoka endapo wamiliki wa klabu hiyo watamtaka kufanya hivyo.
Liverpool imejikuta ikiaibishwa kwa kipigo cha magoli 6-1 kutoka kwa Stoke City ikiwa ni mchezo wa kufungua pazia la ligi kuu ya England jana pamoja na mechi ya mwisho wa nahodha wao Steven Gerrard.
Hata hivyo amesema anasikitishwa na matokeo ya jana ya timu hiyo kufungwa magoli sita na kusema wamedhalilika kwani kwa miaka miangi hawajawi kufungwa idadi kubwa kama hiyo ya magoli na amesisitiza mashabiki wanaitaji kuomba radhi.
 Kwa habari na matukio kemkem usiwe mbali nami, ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment